
Je! Unamkumbuka yule mtu uliyemwona kwenye sherehe akiwa amekunja sura na
anaonekana kuwa na wasiwasi? Bila shaka jibu ni hapana.
Utafiti mpya unaonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa
wa kumkumbuka mtu ikiwa sura yake inalingana na muktadha unaozunguka.
Haijalishi wewe ni mnyonge kiasi gani, mara nyingi huwa ni ngumu kuepuka
nguvu ya tabasamu. Ni tabia ambayo binadamu anazaliwa nayo . Watoto huanza
kutabasamu pindi wanapotimiza wiki 6-8, hata wale ambao wamezaliwa vipofu. Kwa
hivyo ni muhimu kufahamu kuwa tabasamu sio kielelezo tu cha furaha bali
huchukua sehemu kubwa katika muingiliano wetu kijamii.
Tabasamu halijifichi
Jambo moja na la uhakika ni kuwa watu wengi
tumekuwa tukitekwa na tabasamu. Utafiti umeonyesha kuwa sio tu sura
zinazotabasamu zina nafasi kubwa ya kutuvutia, pia zinaashiria uaminifu ,
ujamaa, na umahiri tofauti na sura ya mtu ambayo ipo katika hali ya kawaida.
Tuna uwezekano mkubwa zaidi wa kugundua nyuso zenye furaha. Kwa hivyo, ikiwa
akili zetu huzipa kipaumbele zaidi nyuso zenye furaha, je! ni kweli jambo hili
linaweza kuathiri kumbukumbu zetu pia?.
Kulingana na utafiti wa 2008, watafiti waligundua
kuwa jambo hili linaweza kuwa na ukweli ndani yake.
Tabasamu Kwenye Sherehe na Watu Watakukumbuka Zaidi
Utafiti uliochapishwa mapema mwaka huu ulichunguza
jinsi mazingira ya kijamii yanaathiri kumbukumbu zetu. Washiriki walionyeshwa
picha za sura za watu zikiwa kwenye mazingira tofauti tofauti yale ya furaha na
huzuni kisha baadaye wakapewa picha tu za watu pasi kuonesha
mazinguira waliopo. Uchunguzi ulifuatiwa na wao kuulizwa wanakumbuka nyuso na
ikiwa wangeweza kuoanisha uso na eneo la asili la hapo awali. Utafiti huo ulitoa
matokeo ya kupendeza kwani Washiriki walikumbuka nyuso zenye furaha ambazo
zilionekana kwenye mazingira ya furaha na hata zile zilizoonekana kwenye
mazingira ya huzuni lakini zikiwa zinaonesha furaha zilitambuliwa kwa wingi.
Nyuso zenye woga hazikuwa za kukumbukwa Zaidi.
Kwa hivyo inaonekana wazi. Sio tu kutabasamu
hukufanya ujisikie vizuri, pia ni njia ya kuhakikisha haupotei kwenye
kumbukumbu ya watu unaokutana nao. Hivyo kumbuka, unapotabasamu:
- utaonekana kuvutia Zaidi
- Utaonekana wa kipekee,
- Utaonekana kuwa mahiri na muaminifu na
kutakuwa na
- uwezekano mkubwa wa kukukumbuka
Leave a comment