
Uongozi wa Wilaya ya Poquoson, Virginia imelazimika kumtafuta Ester French (85) ili kumjulisha kuwa wamepata pochi yake iliyopotea karibu miaka 70 iliyopita.
Ester French alikuwa Mwanafunzi wa zamani wa shule ya Poquoson iliyopo Virginia.
Pochi hiyo ilipatikana katika vifusi katika eneo lililokuwa la mazoezi la shule hiyo ambalo lilibomolewa kama sehemu ya mradi wa ukarabati wa shule ya Poquoson .
Pochi
ulikuwa na hali mbaya lakini ilikuwa na vielelezo kadhaa ambavyo vilisaidia
maafisa wa shule kumtafuta mmiliki, Ester French ambaye alikuwa tayari
ameshabadili jina lake.
"Niliposikia
sikuamini," Ester (85), aliiambia shirika la utangazaji la CNN.
Ndani
kulikuwa na picha mbili zilizofifia, stempu za Krismasi kutoka 1951, kalenda za
mwaka huo, na senti 85 za sarafu za fedha, Afisa wa shule hiyo aliwaambia CNN.
Kulikuwa pia na kitabu kidogo cha blue, kipande cha gazeti kinawaomba wasomaji
waombee mabaharia wa Jeshi la Wanamaji wanaohudumu katika Vita vya Korea.
Anasema
hakumbuki kwa nini alihifadhi nakala hiyo, lakini kuna vituo vingi vya Jeshi la
Wanamaji karibu na Poquoson kusini mashariki mwa Virginia.
"Sina
hakika kwanini nilihifadhi nakala hiyo," alisema. "Labda
nitakapoiona, nitajua. Tunazungumza miaka mingi iliyopita, unajua?"
Ester
anakumbuka akiweka mkoba huo kwenye ukingo wa ukumbi wa mazoezi na kugundua
kuwa ulikuwa umeanguka chini ya shimo ambalo lilikuwa chini kabisa kwenye jengo
la matofali.
"Hakukuwa
na cha wakati nilipoipoteza," alisema. "Labda niliripoti wakati huo,
lakini nilijua kuwa sikuweza kuipata na nilikuwa najisikia vibaya wakati
huo."
Msimamizi
wa Shule za Umma za Jiji la Poquoson, Arty Tillett aliiambia CNN kwamba ilibidi
wafanye uchunguzi ili kumpata Ester ambapo hapo baadae walimpata jamaa ambaye
bado anaishi katika eneo hilo.
Ester anadai kuwa tukio hilo limerudisha kumbukumbu nzuri za siku zake za shule, na alipigiwa simu na binamu na mwanafunzi mwenzake ambaye wamefanikiwa kuungana tena baada ya tukio hilo.
Leave a comment