Habari

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam wa kwanza Afrika Kupewa Hati ya Ubora kwa Usalama dhidi ya Covid-19

Uhakiki wa Skytrax ulitazama namna ambavyo taratibu za kukabiliana na Covid-19 katika uwanja wa JNIA zinazingatiwa

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam umekuwa uwanja wa ndege wa kwanza Afrika kupewa hati ya ubora kwa usalama dhidi ya Covid-19 na Shirika la Kimataifa la Viwango vya Usafiri wa Ndege, Skytrax. Uwanja wa JNIA umepewa ubora wa nyota tatu baada ya kufanyiwa uhakiki wa hatua zote za muhimu za kukabiliana na maambukizi uwanjani hapo. 

 

Picha iliyowekwa patika mtandao wa Skytrax ikionesha ushahidi wa taarifa za kujikinga dhidi ya Covid-19 zinazopatikana katika uwanja wa JNIA na hati ta ubora ambayo inaonesha JNIA imepata nyota tatu. 


Uhakiki wa Skytrax ulitazama namna ambavyo taratibu za kukabiliana na Covid-19 katika uwanja wa JNIA zinazingatiwa kwa lengo la kuwakinga watumiaji na watendaji katika uwanja huo. Uhakiki huu ambao ulifanyika Disemba 2020 unaonesha kwamba JNIA wamechukua hatua za msingi za kimataifa za kukabiliana na maambukizi ya Covid-19 ikiwemo kuweka alama za kuelekeza sehemu za kusafisha mikono na alama za kuepusha kukaribiana.