Habari

UVCCM Waomba Radhi, Wahimiza Mshikamano

Akiongea na vyombo vya habari, Jumapili 28, march 2021 Jijini Dodoma, Kheri James alinukuliwa akisema "Kama kuna jambo huko nyuma ambalo kwa maneno ama matendo ambalo litatumika kama rejea ya kuzuia hiyo dhamira ya Rais wetu, sisi tunasema tunaomba radhi"

Mwenyekiti Wa Uvccm Taifa Ndugu Kheri James, Amewaomba Radhi Watanzania kwa niaba ya Uvccm ikiwa waliwahi kukwazwa au kukosewa kwa namna moja ama nyingine na maneno ama matendo ya Uvccm. 

Akiongea na vyombo vya habari, Jumapili 28, march 2021 Jijini Dodoma,  Kheri James alinukuliwa akisema "Kama kuna jambo huko nyuma ambalo kwa maneno ama matendo ambalo litatumika kama rejea ya kuzuia hiyo dhamira ya Rais wetu, sisi tunasema tunaomba radhi na tuko tayari kushirikiana na Rais wetu ili kuhakikisha dhamira yake haikwazwi na matendo wala maneno yetu.’’

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya mazishi ya aliekuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John pombe Magufuli aliyekuwepo madarakani.

Aidha ndugu Kheri james amaeongeza kuwa vijana wanapaswa kuwa kielelezo cha maendeleo ya nchi na kuwa mstali wa mbele kumuunga mkono Rais mpya wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan “Jukumu letu la msingi tunalotakiwa kulifanya kama vijana ni kuhakikisha hii dhamira njema aliyonayo Rais wetu kuhusu umoja wa watanzania, haki zao, usawa wao pamoja na mwelekeo wao kama taifa sisi tunakuwa ndio nguzo imara kuhakikisha haya yanatokea, tusiende tukachochea uadui, chuki, na uhasama na ikiwa yaliwahi kufanyika, sisi tuna haki na wajibu wa kuombana radhi na kuanza upya kama taifa.” Kheri james.

Taarifa hiyo imepokelewa kwa ukosolewaji mkubwa kutoka kwa jamii, ikidaiwa haijaonesha kukiri moja kwa moja makosa ambayo wengi waliyaona huko nyuma, kipindi cha serikali iliyopita.