Maisha

Utafiti: Mbwa Wana Uhusiano Mzuri na Wanawake Kuliko Wanaume

Wanaume Huweza kufuga mbwa kwa ajili ya Ulinzi, lakini ni wanawake ambao huonesha upendo na huruma

Katika utafiti uliochapishwa na Royal Society of Open Science, Marekani ulichunguza mbwa 18 na kurekodi milio yao kwa kujibu hali katika muktadha tofauti tofauti.

Wakati tafiti zingine zimeonyesha kuwa binadamu wanaweza kuelewa mlio wa mbwa, utafiti huo ulikuwa wa aina yake katika kuzingatia milio.

Watu arobaini waliulizwa kutambua kila kilio kilimaanisha nini, yaani, woga, uchokozi, furaha, kukata tamaa, au michezo. Asilimia 63 ya washiriki waliweza kutambua kwa usahihi ni kwa nini mbwa alikuwa akibweka. Kati ya asilimia 63 hiyo, wanawake walifanya vizuri zaidi kuliko wanaume, na kama inavyotarajiwa, wale wanaoishi na mbwa majumbani walifanya vizuri zaidi kuliko wale ambao hawana.  

Kwa nini wanawake walifanya vizuri?

Utafiti ulionesha kuwa wanawake wana huruma na hisia kuliko wanaume. Kulingana na tafiti hiyo, wanawake wanaweza huwa na huruma zaidi na wenye hisia kali kwa wengine na hii inawasaidia kuhusisha zaidi muktadha huohuo pindi wanapokuwa karibu na mbwa.

Utafiti huu sio wa kwanza kuthibitisha kuwa mbwa anaweza kuwa rafiki bora wa wanawake. Mnamo Disemba, utafiti mwingine uliohusisha washiriki 1,000 kutoka Marekani uligundua kwamba wanawake hulala vizuri karibu na mbwa kuliko watu wengine. Kulingana na utafiti huo, iligundulika kuwa mara nyingi mbwa hakatizi usingizi wa mtu tofauti ukilala karibu na mtu na pia huwapa binadamu hisia za faraja na usalama tofauti na pindi ukilala na mwenza wako.

Inasemekana hapo awali kipindi mbwa walianza kuishi na binadamu ni wanawake ambao walianza kuwapa mbwa majina, kuwaacha walale ndani ya nyumba, na waliomboleza walipokufa. Wanaume wanaweza kuwa wamefuga mbwa kwa ajili ya Ulinzi, lakini ni wanawake ambao waliwaonyesha upendo na huruma.