Duniani

Sera ya Uwazi Yaigonganisha Serikali ya Ukraine na Makampuni ya Chanjo ya Corona

Ukraine inalazimika kuachana na sheria ya uwazi kwani makampuni makubwa yanayosambaza chanjo ya corona yanataka sheria hiyo ibadilishwe ndipo waweze kupewa dawa

Baada ya mapinduzi miaka saba iliyopita nchini Ukraine, raia wamegundua kuwa rais aliyeondolewa madarakani (Viktor Yanukovych) alitumia pesa za umma kujijengea jumba kubwa na hifadhi ya wayama binafsi, uwanja wa gofu na karakana iliyojaa magari ya kale.

Ili kuzuia ufisadi huo siku za usoni, mageuzi yalifanyika yakihusisha mikataba yote ya serikali kutangazwa kwa umma.

Marekebisho hayo ambayo yalionekana kama mafanikio adimu kuwahi kutokea katika harakati za kukomesha ufisadi nchini, yalifanikiwa pia kuingiza mamilioni ya dola katika mikataba ya ununuzi wa vifaa tiba kila mwaka.

Lakini hivi sasa Serikali ya Ukraine inalazimika kuachana na sheria hiyo kwani makampuni makubwa yanayosambaza chanjo ya corona yanataka sheria hiyo ibadilishwe ndipo waweze kupewa dawa.

Katika kujadiliana na serikali, kampuni za dawa zikiwemo Pfizer, Moderna na Johnson & Johnson wamesisitiza kuwa masharti mengi ya mikataba hiyo yanahusu siri za biashara hivyo ni lazima mikataba hiyo ifanyike kwa siri.

Hitaji hilo la makampuni ya dawa kwa Ukraine yameiweka serikali katika wakati mgumu na kupelekea kampuni ya serikali inayohusika na manunuzi ya dawa kuwa katika sintofahamu kwani sheria ya nchi inawahitaji waweke wazi mikataba yote ya manunuzi.

Ili kuzuia ufisadi huo siku za usoni, mageuzi yalifanyika yakihusisha mikataba yote ya serikali kutangazwa kwa umma.

Marekebisho hayo ambayo yalionekana kama mafanikio adimu kuwahi kutokea katika harakati za kukomesha ufisadi nchini, yalifanikiwa pia kuingiza mamilioni ya dola katika mikataba ya ununuzi wa vifaa tiba kila mwaka.

Lakini hivi sasa Ukraine inalazimika kuachana na sheria hiyo hatua ambayo serikali inadai kuwa inalazimika kwani makampuni makumbwa yanayosambaza chanjo ya corona ndiyo yanataka iwe hivyo.