Tanzania

Ujumbe wa Shukrani Kutoka kwa Tanasha Kwenda kwa Baba mtoto Wake

Mwimbaji Tanasha Donna Oketch ameandika ujumbe wa shukrani kwa baba mtoto wake Diamond Platnumz baada ya wimbo wake unaofahamikakama ‘Gere’ kuonekana kwenye orodha ya nyimbo 10 za zilizotazamwa zaidi kwenye YouTube mnamo 2020, Afrika. Bi Donna alitoa shukrani kwa Chibu Dangote kwa kumuamini na kukubali kushiriki katika wimbo wake #GERE ambao unaonekana nambari saba kwenye orodha na ukiwa na watazamaji  zaidi ya milioni 22.


Baada ya kuona ujumbe huo Platnumz alijibu “MoMy ya NJ !!! 🔥⛽🚬 ”. Tanasha Donna na Diamond Plutnumz

Gere ambayo ilitoka mnamo 19 Februali 2020 ilifanikiwa kutazamwa na watu milioni 1 ndani ya masaa 14.

Kwenye orodha hiyo ya nyimbo 10 zilizotazamwa zaidi kwenye YouTube mnamo 2020 ni Diamond na wimbo wake Jeje ambao unawatazamaji zaidi ya milioni 41, #jeje iliyotolewa mnamo Feb 26, 2020.Mwanamziki wa Kenya mwingine ni Otilie ambaye wimbo wake wa DUSUMA aliomshirikisha mwanamziki Meddy kutoka Rwanda umekaa nafasi ya nane ukiwa na watazamaji zaidi ya milioni 19.

Orodha yote ya nyimbo zillitizamwa Zaidi Afrika

1.   Jeje - Diamond Platnumz –Tanzania ( watazamaji 41.2 M)

2.   Duduke- Simi- Nigeria (over 29 M views)

3.   Waah- Diamond Platnumz Ft Koffi Olomide (Tanzania) (watazamaji 25 M)

4.   Nobody- DJ Neptune, JoeyBoy, Mr Eazi (Nigeria/Ghana)- watazamaji 25 M)

5.   Vibration- FireBoy DML- Nigeria (watazamaji 23 M)

6.   Teamo- Rayvanny –Tanzania- (watazamaji 22 M)

7.   Gere- Tanasha Donna ft Diamond Platnumz – Kenya/Tanzania-  (watazamaji 22 M)

8.   Dusuma- Otile Brown ft Meddy- Kenya/Rwanda-( watazamaji 9 M)

9.   Olandi- InossB- DRC Congo – (watazamaji 17 M )

10.   Shekere- Yemmi Alade ft Angelique Kidjo- Nigeria/ Benin- (watazamaji 16 M views).

11.  Msanii wa nyimbo wa Nigeria Semi anashika nafasi ya pili na wimbo wake Duduke (Zaidi ya maoni 29M), wa tatu ni Waah na Diamond ft Koffi Olomide (zaidi ya maoni milioni 25)