Duniani

Ufilipino: Mwanaume Mmoja Afariki Baada ya Polisi Kumrusha Kichura Mara 300 kwa Kosa la Kukiuka Amri ya Kutotoka Nje

"Alisema waliokutwa nje walilazimishwa kuruka kichura mara 100 kwa Pamoja na kama kuna mtu atabaki nyuma basi wote mtarudi kuanza upya" Mke wa Penaredondo, Balce alisimulia kama alivyohadithiwa na marehemu mumewe.

Alhamisi iliyopita Darren Manaog Penaredondo umri miaka 28, alikuwa nje akinunua maji katika duka wakati aliposimamishwa na wanamgambo wa eneo hilo kwa kukiuka amri ya kutotoka nje pindi inapotimu saa 12 jioni

Mke wa marehemu, Balce amedai kuwa Penaredondo alirudishwa nyumbani asubuhi saa 2 akiwa hawezi kutembea vizuri hadi kulazimika kutambaa, siku iliyofuata alipata mshtuko na moyo na kufariki muda mfupi baadaye

"Alisema waliokutwa nje walilazimishwa kuruka kichura mara 100 kwa Pamoja na kama kuna mtu atabaki nyuma basi wote mtarudi kuanza upya" Balce alisimulia kama alivyohadithiwa na marehemu mumewe.

Mkuu wa polisi wa eneo ambalo tukio hilo limeripotiwa ameondolewa kwenye wadhifa wake baada ya vuta n’kuvute kwani hapo awali alidai kwamba wanaokiuka amri ya kutotoka nje walikuwa wakipelekwa kufanya huduma za kijamii na sio kufanya mazoezi ya mwili kama adhabu.

Miji mingi Ufilipino kwa sasa imefungwa kutokana na kuongezeka kwa kesi za maambukizi ya virusi vya corona na miji hiyo imewekewa amri ya kutotoka nje usiku kuanzia saa 12 jioni hadi 5 asubuhi.