
Rais anayeondoka wa Marekani Donald Trump amesema vizuizi dhidi ya wasafiri kutoka Ulaya na Brazil vitaondolewa kuanzia Januari 26, ijapokuwa utawala unaoingia madarakani wa Biden umejibu kuwa vizuizi hivyo vitaendelea kutekelezwa.
Trump, ambaye amebaki na
chini ya saa 21 kabla ya kuondoka madarakani, amesema katika tangazo kuwa
kuingia bila vizuizi nchini Marekani kwa watu ambao wamezuru eneo la Ulaya la
Schengen, Uingereza na Brazil hakuna tena madhara kwa maslahi ya Marekani.
Trump amesema uamuzi huo
umechukuliwa kutokana na ushauri wa kiafya, baada ya Shirika la Kudhibiti na
Kuzuia Magonjwa nchini Marekani (CDC) kutoa amri kuanzia Januari 26, inayowataka
abiria wote wa ndege wanaoingia Marekani kutoa ushahidi wa vipimo vya corona.
Muda mfupi baada ya tangazo hilo, msemaji wa Rais Mteule wa Marekani Joe Biden
akasema utawala unaoingia hauna nia ya kuondoa vikwazo vya safari za kimataifa.
Machi mwaka jana,
utawala wa Rais Trump uliweka marufuku ya kuingia kwa wasafiri kutoka Uingereza
na Ireland ikiwa ni juhudi za kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.
Mnamo Mei, Trump
alizuia uingiaji wa raia wasio wa Wamarekani wanaosafiri kutoka Brazil, nchi
inayoongoza kwa maambukizi zaidi ya virusi vya corona Marekani Kusini na sasa
ni nchi ya 3 yenye idadi kubwa ya maambukizi ikiwa na visa vya maambukizi
vinavyozidi milioni 8.4.
Siku hiyo marufuku itakapoondolewa, Marekani itaanza kuhitaji abiria wote wanaosafiri kuingia nchini kwa ndege za kimataifa kupima COVID-19.
Leave a comment