Habari

Trump Avunja Ukimya Muda Mchache Kabla ya Kuondoka Madarakani

Katika video aliyoiweka kwenye mtandao wa YouTube, alisema "mapambano yalikuwa makali, vita ilikuwa ngumu... kwasababu hicho ndicho mlinichagua kukifanya"

Rais Donald Trump amelihutubia taifa la Marekani kabla hajaondoka madarakani na kusema: "Tumefanya kile ambacho tulikuja kukifanya na tumefanya mambo mengine mengi."

Katika video aliyoiweka kwenye mtandao wa YouTube, alisema "mapambano yalikuwa makali, vita ilikuwa ngumu... kwasababu hicho ndicho mlinichagua kukifanya".

Trump ameeleza kuwa, wamejenga Uchumi Bora zaidi katika historia duniani akiongeza kuwa, amekabiliana na vita ngumu kwa kuwa hicho ndicho alichochaguliwa kufanya

Rais huyo wa 45 wa Marekani pia ameutakia mafanikio Utawala unaokuja. Joe Biden ambaye alimshinda Trump katika Uchaguzi Mkuu wa Novemba 2020 anatarajiwa kuapishwa leo

Aidha, Rais Trump leo ametoa msamaha kwa watu 73, akiwemo msaidizi wake wa zamani, Steve Bannon na washirika wake wengine, masaa machache kabla ya kuondoka ofisini. Taarifa kutoka Ikulu ya White House inasema kuwa Trump alitoa msamaha huo na kubadilisha hukumu ya watu wengine 70 zaidi. Bannon alipewa msamaha huo baada ya kushtakiwa kwa kulaghai watu kuhusu pesa zilizokusanywa kujenga ukuta wa mpaka wa Mexico ambayo ilikuwa sera kuu ya Trump. Taarifa hiyo iliongeza kuwa Bannon amekuwa kiongozi muhimu katika harakati za kihafidhina na anajulikana kwa ustadi wake wa kisiasa. Vyombo vya habari nchini Marekani awali vilikuwa vimeripoti kuwa rais huyo alifanya maamuzi ya dakika za mwisho baada ya kuzungumza na Bannon kwa njia ya simu.

Wengine kati ya watu kadhaa wanaosamehewa ni rapa Lily wyne na Kodak Black ambao walihukumiwa kwa makosa ya kumiliki silaha bila kibali.

Bwana Trump anaondoka madarakani akiwa bado hakubaliani na matokeo ya uchaguzi wa Novemba, ambao ulimuibua Joe Biden kuwa rais.

Rais Mteule, Joe Biden na makamu wake Kamala Harris wataapishwa leo Jumatano.