
Nchi ya Somalia siku ya Jumanne iliiambia Mahakama ya
Umoja wa Mataifa kwamba suala la Kenya kumiliki eneo lenye ukumbwa wa
kilomita za mraba 160,000 katika bahari Hindi lilitokea baada ya Kenya kutia
saini makubaliano na Tanzania mnamo Julai 2009 ambayo yalipelekea nchi ya
Tanzania kupata sehemu kubwa zaidi baharini hivyo wao kusogea kumega sehemu ya
Somalia.
Mahakama ilisema kwamba makubaliano ya mpaka kati ya Kenya
na Tanzania yaliiiponza Kenya kwani sehemu ya umiliki wake ilipunguzwa.
Mawakili wa Somalia walisema makubaliano ya
mipaka ya baharini ya Kenya na Tanzania ya mwaka 2009 yalitiwa saini wakati
Kenya ikijua wazi kwamba Somalia inadai nafasi yake baharini. Athari za
makubaliano ni kwamba walipunguza haki ya umiliki wa mpaka wa bahari upande wa Kenya,
Mahakama ilielezwa.
“Kenya ilijiponza yenyewe ilipofanya makubaliano na
Tanzania. Kwa hiari yake ilipoteza haki zake.
Iliamua kuipa Tanzania kilomita za mraba 25,000 za nafasi
yake ya baharini. Kenya haina haki ya kuifanya Somalia ilipe kile ilichofanya
na Tanzania kwa kurekebisha mipaka,”wakili hao walisema.
Wakati wa siku ya pili ya kusikilizwa kwa kesi hiyo bila
uwepo wa Kenya, Mahakama iliambiwa kwamba Kenya ilikuwa imesema kuwa katika
makubaliano hayo ilikuwa inalinda maslahi yake na usalama ambapo walijibiwa na
mawakili kuwa itakuwa hatari kuibiana mipaka kati ya nchi kwa kigezo tu cha
nchi gani ina nguvu, wakisisitiza kuwa Somalia ina haki sawa katika mipaka.
Waliongeza kuwa hata ikitokea Kenya ikaumia ikitokea
Somali wakapewa eneo la baharini linalogombaniwa basi hakutokuwa na upendeleo.
Mawakili hao pia waliambia mahakama kwamba Kenya katika
hoja zake ilitaka mahakama itumie mkondo wa mstari wa usawa nba umbo la pembe
tatu kutoka wakati ambapo nchi hizo mbili zilikutana eneo la pwani katika
kuamua mzozo huku Somalia ikisema mpaka wa majini unastahili kufuata mpaka ya
ardhini. Walakini, mbinu hiyo haijazoeleka na haitumiki katika masuala ya
mipaka. Mawakili hao walisema mbinu hiyo haijawahi kutumiwa na mahakama yoyote
na ICJ itakuwa ya kwanza kufanya hivyo.
Wakati wanaelezea Somalia kama nchi ya dhaifu na moja ya
nchi masikini zaidi ulimwenguni kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe,
mawakili waliiomba mahakama kuzingatia haki za nchi hiyo kulingana na jambo
hilo na kutambua ukiukaji wa haki zake unaofanywa na nchi ya Kenya.
Pia mawakili hao walitaka mahakama iamuru Kenya iache
kukiuka haki za kujitawala za Somalia.
"Somalia inataka kutetewa kwa haki zake. Rasilimali
ni muhimu kwa maendeleo yake na mustakabali wa watu wake. Somalia ilifika
mahakamani kwa ajili ya kulinda haki zake,” wakili hao walisema kwa
wanapomaliza kuwasilisha madai yao.
Rais wa mahakama alisema ICJ imepokea barua kutoka Kenya ikijibu
madai ya Somalia. Barua hizo zinahusu kutoshiriki kwa Kenya katika vikao.
Jaji alisema barua imepokelewa na mahakama itazungumza baadae.
Chanzo: Afro News
Leave a comment