
Mashambulio hayo yametokea mapema
asubuhi ya leo yakilenga kambi za jeshi katika miji ya Barire na Awdhegle
kusini mwa Somalia. Mashambulio yalianza na mabomu ya gari ya kujitoa muhanga
katika vituo vyote viwili, likifuatiwa na shambulio la kambi za wanajeshi.
Afisa wa jeshi, Hussein Nur alinukuliwa
akisema “jeshi lilipoteza askari kadhaa katika shambulio hilo la vituo vya
Bariire na Awdhigle.” bila kutoa nambari sahihi ya vifo vya askari
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba
wanajeshi kutoka kambi mbalimbali walienda kutoa msaada katika kambizilizoathiriwa na
kufanikiwa kuwaua wanamgambo kadhaa wa kikundi cha Al-Shabab ambacho
kilitekeleza shambulio hilo.
Baada ya mapigano hayo Jeshi
sasa linadhibiti vituo vyote viwili na maeneo ya karibu huku likianzisha msako
maalumu. "Tunawafuata wanamgambo katika msitu unaozunguka." Afisa
Hussein Nur Alisema
Kundi la kigaidi la Al-Shabab
limekuwa likianzisha mashambulio kwa miaka kadhaa nchini Somalia wakitaka nchi
iongozwe kwa misingi ya kidini.
Leave a comment