
Shirikisho la mpira wa miguu
barani Afrika (CAF) limetoa hukumu juu ya rufaa iliyofunguliwa tarehe 21/3/2021
na timu ya mpira wa miguu ya Al Merrikh inayoshiriki ligi ya mabingwa ya Afrika
kutoka nchini Sudani.
Kupitia Barua iliyotumwa tar
28 march 2021 kwa shirikisho la mpira wa miguu la nchini Sudan kuelezea hukumu
hiyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika limesema “linatambua vipimo
vya corona vilivyochukuliwa masaa 48 kabla ya mchezo huo na si vipimo vingine
kama vile vilivyochukuliwa siku moja ama zaidi baada ya mchezo, kwani vipimo
hivyo huwa na tabia ya kubadilika”.
Aidha shirikisho hilo la soka
barani Afrika limesema hawawezi kuingilia utaratibu wa utoaji taarifa kuhusu
corona kwa nchi yeyote kwani nchi hizo huwa na utaratibu maalumu wao wa
kuzisimamia taarifa hizo.
Al Merrikh ilifungua
mashitaka dhidi ya Simba ikiwatuhumu kufanya udanganyifu kuwa klabu ya Wekundu
wa Msimbazi Simba walitoa majibu yasiyo sahihi kwa baadhi ya wachezaji wa timu
hiyo ya Al Merrikh siku mbili kabla ya mchezo hivyo kuwafanya Al Merrikh
kushindwa kuwatumia wachezaji hao kwenye mchezo uliochezwa 16/03/2021 kwenye
uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam nchini Tanzania, ambao simba walishinda
goli 3 wakati Al merrick hawakupata kitu.
Kutokana na ushindi wa kesi
hiyo, Klabu ya Simba inaendelea kubaki kileleni katika kundi A wakiwa na alama
kumi (10), hivyo kuwafanya kutafuta alama moja (01) tu ili waweze kutinga hatua
ya robo Fainali ya michuano hiyo.
Aidha jumapili alasiri tarehe
3/4/2021 Simba inatarajiwa kushuka dimbani dhidi ya timu ya As vita club kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika uwanja wa Benjamini Mkapa, huku siku
baadae tarehe 9/4/2021 ikienda kumalizia na timu ya al ahly nchini Misri.
Leave a comment