Habari

Shepherd Bushiri, Muhubiri Tajiri Aliyetoroka Afrika Kusini kwa Tuhuma za Utakatishaji Fedha Amekamatwa Nchini Malawi

Anakabiliwa na mashtaka 419 yakiwamo makosa ya wizi wa mamilioni ya dola na utakatishaji wa fedha.

Na Jackline Mgeni

Muhubiri mwenye Ukwasi, Shepherd Bushiri amekamatwa nchini Malawi alikokimbilia kukwepa mashtaka yanayomkabili, huku akikikiuka masharti ya dhamana aliyopewa nchini Afrika Kusini.


Nabii Huyo anakabiliwa na mashitaka 419 ikiwa ni pamoja na wizi wa mamilioni ya dola na kuhusika na ufisadi  nchini Afrika kusini.

Yuko Malawi kutafuta haki, ambayo anaamini asingeweza kuipata akiwa  Afrika Kusini

Polisi wa Malawi walianzisha msako kwa mtuhumiwa huyo Jumanne baada ya Polisi nchini Afrika kusini kutoa kibali cha kukamatwa wahalifu hao.

 

"Nabii huyo na mkewe walijisalimisha kwa polisi, huko Lilongwe mnamo Jumatano, Novemba 18, 2020 baada ya kugundua kuwa wapo chini ya msako," msemaji wa polisi James Kadadzera alisema katika taarifa na kuongeza kuwa wenzi hao watapelekwa kortini.

 

Msemaji wa Bushiri, Ephraim Nyondo, alikanusha taarifa zinazosambaa kuwa kukamatwa kwa wenzi hao kulisababishwa na kibali hicho huku yeye akieleza kwamba Bushiri alikuwa ameapa kujisalimisha  kwa Polisi wa Malawi ili kuthibitisha hakimbii mkono wa dola

 

"Yuko Malawi kutafuta haki, ambayo anaamini asingeweza kuipata akiwa  Afrika Kusini," Nyondo alisema.

 

Bushiri, ambaye anapata utajiri wake kupitia michango kutoka kwa wafuasi wa kanisa lake la Enlightened Christian Gathering huko Pretoria, anadai kwamba anahofia usalama wa maisha yake nchini Afrika Kusini.

 

Mamlaka ya Afrika Kusini, ambayo ipo katika harakati kutaka kujua jinsi Bushir alivyoondoka nchini humo, wameanzisha kesi za kisheria ili kuhakikisha anarudi kuhukumiwa nchini Afrika kusini. Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zinasema kuwa Bushiri pamoja na mke wake walitoroshwa kupitia msafara wa Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera ulioenda nchini humo kwa ziara ya kikazi.


Hata hivyo, Msemaji wa Ikulu ya Lilongwe amesema kuwa Rais Chikwera wala serikali haihusiki na utoro huo wa nabii huyo ambaye maisha yake yamegubikwa na utata na kashfa mbalimbali kuhusu imani na umilikin wa mali