
Rais Samia suluhu ameiagiza
Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni pamoja na Wizara ya Teknolojia na
Mawasiliano kuvifungulia na kuviondolea adhabu vyombo vyote vya Habari
vilivyofungiwa kwa makosa mbalimbali.
Rais ametoa maagizo hayo leo
tarehe 06/04/2021 Ikulu Dar es salaam, alipokuwa akiwaapisha Watendaji wa Wizara mbalimbali wakiwamo Makatibu Wakuu, Manaibu pamoja na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali.
Katika hotuba yake Rais
amesema “wizara ya Habari nasikia kuna vyombo vya Habari mmevifungia,
vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya serikali, tusiwape Uhuru wa
kusema tunabinya vyombo vya Habari, tusifungie tu kibabe.” Samia Suluhu Hassan
Wananchi wamedai kuwa maagizo
hayo yanaleta sura mpya ya uhuru wa vyombo vya habari ambao ulilalamikiwa
kubanwa sana kipindi cha mtangulizi wake, Hayati. John Pombe Magufuli.
Aidha, katika mitandao ya jamii, watu wamepongeza hatua hiyo huku wakija na ombi la kutaka kurekebisha sheria za vyombo vya habari ambazo zilitungwa na zimekuwa kandamizi kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini.
Asante @SuluhuSamia kufungulia vyombo vya habari
Rais wetu leo umewapa matumani makubwa watanzania. sisi watanzania tuko pamoja na wewe . umekonga miovyo yetu. sisi kazi yetu kukuombea usiku na Mchana Mungu akulinde na kutunza Afya yako . Hakika kiatu kimekutosha kabisa. Mama yetu watanzania wanakupenda.
— Michael Bante (@BanteMichael) April 6, 2021
Leave a comment