Maisha

Saikolojia Inayozunguka Tabia ya Manunuzi ya Kimhemko

Wafanyabiashara hufurahi pindi tiunapofanya manunuzi ya bidhaa zao, lakini aina hii ya ununuzi ni matokeo ya udhaifu wetu kisaikolojia

Ununuzi wa mhemko hufanyika wakati tunapotaka kuonesha tunajijali sana au kukutana na vitu vinavyokuhamasisha kufanya manunuzi, mfano punguzo la bei na ofa katika maduka. Lakini ni nini kingine kinachotufanya tuwe katika hali ya kufanya manunuzi bila mpangilio?

Utafiti unasema kuwa ni mambo mengi.

Je! Una uwezo wa kuishinda nguvu hii?

Kama watumiaji, kawaida tunaamini kwamba tuna uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kujua kipi tunataka kununua na kipi hatuhitaji.

Lakini wanasaikolojia ambao wanachunguza tabia hii ya wanunuzi wanadhani kuwa kuna mambo mengi yanayoizunguka tabia hii.

Utafiti wa watumiaji unaonesha mhemko huu mara nyingi hupelekea watu kununua vitu ambavyo hawakupanga kununua, vitu ambavyo hawavihitaji, na hata vitu ambavyo hawana hakika ikiwa wanavitaka.

Kwanza, wanunuzi wa aina hii wanajali zaidi taswira yao katika jamii, hivyo wengi wao hufanya manunuzi ili waonekane wazuri machoni pa wengine. Pili, wanunuzi hawa huwa na shida katika kutawala hisia zao hali ambayo kusababisha iwe ngumu kwao kupinga msukumo wa wa kutumia pesa ghafla. Tatu, wanunuzi wa msukumo huwa na furaha kidogo, na kwa hivyo wanaweza kununua kama njia ya kuboresha furaha yao. Mwisho, wanunuzi wa aina hii wana uwezo mdogo wa kufikiria matokeo ya matumizi yao.

Sababu za kawaida za ununuzi wa msukumo

Sayansi inapendekeza kuwa ununuzi wa kimhemko unaweza kusukumwa na sababu kadhaa tofauti:

1. Kujifurahisha

Wakati mwingine, watu hufanya manununuzi ya vitu ili kujifurahisha. Fikra ya furaha utakayoipata pindi utakapoona kitu kipya kwenye oradha ya vitu unavyovimiliki huweza kumfanya mtu afanye manunuzi ya namna hii hasa pindi anapokuwa amefadhaika. Wengi huamini kupata kitu kipya huweza kufanya siku yako mbaya kuwa nzuri au kukuondolea uvivu ambao unaweza ukawa umeamka nao. Hii huweza kuelezea hali yangu kwani huwa ni mvivu kufua nguo hadi pale napokuwa nmetoka mtumbani ambapo kitendo cha kufuya nguo nlizozinunua mtumbani  hunifanya nifue na nguo zangu  chafu zote nilizonazo ndani.

2. Hofu ya kukosa

Ni mara ngapi huwa unaanguka kwenye mtego wa "nunua viwili, pata kimoja bure" au punguzo la bei ambalo hukaa kwa kipindi kifupi? Iwe ni fulana au mafuta mara nyingi watu huchukua vitu ambavyo hawahitaji kwakuwa hawana hakika kama vitapatikana kila wakati. Fikra ya kwamba tunapata vitu vingi kiwango sawa cha pesa ambacho tumezoea kutumia kunua kitu hicho hupelekea watu wengi kufanya manunuzi ya mhemko hata kama wakiwa kwenye mpango wa kuweka akiba.

 3. Haja ya kuhifadhi

Kama buinadamu lazima uwe na hofu ya kuishiwa vitu ambavyo wewe unahisi ni muhimu; tuna tabia ya kurundika vitu tunavyohisi tunapaswa kuwa navyo, hali hii huzidi pindi tunapokutana na bidhaa ambazo huwa hazikai muda mrefu  sokoni na msimu wake ukipita basi huwa adimu na bei yake huiwa ni tofauti na ile ya awali.

4. Tathmini mbaya ya matumizi

Sisi ni watu wenye matumaini makubwa. Tunaamini  kwamba tutakula chakula chote tunachonunua, kuvaa kila nguo, na kutumia vitu vyote vya nyumbani tunavyonunua. Haijalishi umeambiwa na umeshuhudia mara ngapi kuwa jambo hili haliwezi kutokea.

Ni nani ambaye huwa kwenye hatari ya kufanya manunuzi ya mhemko?

Watu ambao kwao kufanya manunuzi huwapa faraja wana uwezekano wa kuwa na tabia ya kununua kwa mhemko. Sisi sote tunataka kupata raha, ni wazi kuwa ni raha kwenda sehemu ya manunuzi na kufikiria raha utakayoipata pale utakapomiliki bidhaa unazoziona. Mara tu tunapoanza kupata raha kama matokeo ya hisia hii ya umiliki, tuna uwezekano mkubwa wa kununua bidhaa hizo ili tuweze kuendelea kupata raha hiyo.

Wakati tumeunganishwa na bidhaa, akili zetu kimsingi zinaanza kutufanya tujione kama tunamiliki bidhaa hizo hali ambayo inafanya iwe ngumu kuondoka bila kununua bidhaa hiyo. Hii inaleta swali, "Je! Muungano huu kati ya binadamu na bidhaa huundwaje?" Uunganisho wa mwili na bidhaa huundwa pindi tukiwa karibu nayo na tunapoweza kuigusa. Uungano wa muda mfupi huundwa wakati tunapohisi tunauwezo wa kununua bidhaa hiyo mara moja. Mwishowe, uhusiano wa kijamii na bidhaa huundwa tunapoona mtu akiitumia bidhaa hiyo hali ambayo hutujengea taswira binafsi tukijilinganisha na bidhaa hiyo.

Watu wenye msongo wa mawazo pia wapo kwenye hatari zaidi ya kufanya manunuzi ya kimhemko ili kutoroka hisia hizo. Inasadikika manunuzi ya namna hii huwapa watu hawa furaha  kuboresha hisia zao ingawa huwa haidumu. Kwa watu wa namna hii, msongo wa mawazo huongezeka pindi watakaposhindwa kununua bidhaa wanayohisi wanataka kuimiliki. Kwao, ununuzi wa mhemko hutazamwa kama njia ya kukabiliana na mafadhaiko. Kwa hivyo, inaaminika kuwa athari ya mafadhaiko itahusishwa vyema na uwezekano wa kushiriki katika manunuzi ya mhemko.

Njia rahisi ya kujua ikiwa ununuzi wako ni wa kimhemko ni kujiuliza, "Je! Nilikuwa na mpango wa kununua bidhaa hii, au nimepata hamu ya kuinunua muda huu?" Ikiwa haukupanga kuinunua, labda umepata ununuzi wa msukumo na ukaamua kuirudisha bidhaa sehemu ilipokuwa ,utakuwa umejiokoa  kwani utakuwa umekataa wazo lisemalo  kununua bidhaa hiyo utakuwa na furaha zaidi, utaheshimiwa zaidi, au utajihisi mkamilifu zaidi. Kwa kufanya hivyo, haitakusaidia tu kuhifadhi pesa yako bali utakuwa mtu ambaye unaweza kutawala hisia zako vema.