Habari

Rais Samia: TAMISEMI Nataka Walimu Wapya 6,000 Waajiriwe, Shule 26 za Kike Zikamilike Mapema Ifikapo 2025

Taarifa hizo zimepokelwa kwa mikono miwili kwa wananchi huku wakidai ni tumaini jipya kwa kupunguza ukosefu wa ajira nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Na Serikali Za Mitaa (TAMISEMI), pamoja na Wizara ya Ofisi Ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuajiri walimu 6,000 mapema iwezekavyo.

 

Ametoa maagizo hayo leo Aprili 6, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kuwaapisha watendaji wa wizara ambao ni makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali za serikali.

 

Akizungumnza katika halfa hiyo Rais Samia amesema “natambua kuwa kuna walimu wengi tu karibu 6000 au zaidi ambao wameacha kazi, wengine wamestaafu na wengine wamefariki, Utumishi na TAMISEMI naomba walimu 6000 wapatikane haraka sana ili wakatoe huduma.”

 

Taarifa hizo zimepokelwa kwa mikono miwili kwa wananchi huku wakidai ni tumaini jipya kwa kupunguza ukosefu wa ajira nchini.

 

Rais Samia ameiagiza TAMISEMI kukamilisha ujenzi wa shule za wasichana 26 nchi nzima ifikapo 2025.

 

Mradi huo umelenga kuboresha mazingira ya watoto wa kike nchini katika kupata haki ya elimu ili kuweza kuleta uwiano sawa wa haki ya kupata masomo kwa watoto wa kike na kiume.

 

Aidha, Wananchi wamependekeza Serikali kuendelea kuajiri na kuboresha mazingira ya elimu nchini ili kutengeneza Zaidi Wataalamu wengi ambao wataweza kushindana kimataifa na kuisaidia Nchi kupiga Maendeleo.