
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo tarehe 01/04/2021 amewaapisha Katibu Mkuu
Kiongozi pamoja na Mawaziri, Manaibu Waziri wa Wizara mbalimbali aliowateua hapo
jana tarehe 31/03/2021 Ikulu Chamwino.
Akizungumza mara baada ya
uapisho huo Rais Samia Suluhu ameionya Wizara ya Fedha kutumia nguvu na vitisho
kukusanya Kodi na hivyo kuleta usumbufu mkubwa kwa ufanyaji wa Biashara nchini
kuwa mgumu na kupelekea kuua Biashara nyingi nchini Tanzania.
Pia Rais ameiagiza Wizara
ya Fedha kwenda kuweka Mazingira bora ya ukusanyaji wa Fedha ikiwa ni pamoja na
kuongeza vyanzo vya Kodi na sio kuweka kodi kubwa ambazo zitaumiza
wafanyabiashara, Mhe. Rais amesema “Waziri wa Fedha katanue wigo wa kukusanya Kodi,
hii mbinu mnatumia sasa hivi ya maguvu na vurugu mnaua walipa Kodi, mnaua
Biashara”
Aidha, Rais ameitaka Wizara
ya Fedha kukusanya Kodi na Mapato ambapo ameitaka Wizara ya Fedha kukusanya
kiasi cha zaidi ya shillingi trillioni 2 kwa mwaka.
Leave a comment