Habari

Picha na Video na NASA Kutoka Sayari ya 'Mars'

Kwa jumla, timu ilisema wamepokea zaidi ya GB 30 za taarifa, na zaidi ya picha 23,000 za asili ya vyombo vya moto vilivyotua

Tukio hilo lina kuja siku nne baada ya Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) kufanikiwa kuwezesha kutua salama kwa chombo chake cha Perseverance rover katika  kreta karibu na ikweta ya sayari hiyo.

"Picha hizi ni matokeo ya ndoto zetu," Al Chen, Kiongozi aliyeongoza kutua kwa chombo hicho alisema.

Picha kutoka kwa kamera zenye kiwango cha juu zilianza kuchukua maili saba kutoka juu ya uso wa Mars, ikionyesha kuyumba kwa nguvu kwa parachute ikifuatiwa chombo cha perverence rover kugusa kwenye kreta.

Kipaza sauti kutoka kwenye chombo hicho pia kimetoa rekodi ya kwanza ya sauti kutoka katika sayari hiyo.

Picha moja ya kustaajabisha ilionesha kutawanyika kwa miamba yenye giza ikiwa miepesi na yenye mashimo. "Tunatumia maneno haya ya jumla katika hatua hii ya awali mpaka tutakapopata na data zaidi ambayo inatuwezesha kupima nadharia zetu na kutoa tafsiri zenye ujasiri zaidi," alisema Ken Williford, kiongozi wa mpango huo 

Kwa jumla, timu ilisema wamepokea zaidi ya gigabytes 30 za habari, na zaidi ya picha 23,000 za asili ya vyombo vya moto vilivyotua.

"Najua umekuwa mwaka mgumu kwa kila mtu na tunatumai kuwa labda picha hizi ... zitawafurahisha watu," alisema Justin Maki, mwanasayansi wa picha.

Chombo hicho chenye magurudumu 6 sasa kitakuwa kwenye sayari hiyo kwa takriban miaka miwili katika mabonde ya eneo hilo, kikitafuta ushahidi unaonesha shughuli za maisha ya awali.

Ikweta ya Jezero inadhaniwa kwamba imekuwa na ziwa kubwa kwa miaka bilioni kadhaa iliyopita.

Na mahali ambapo kumekuwa na maji, kuna uwezekano mkubwa kulikuwa na maisha yalioendelea eneo hilo.