Michezo

Mtanzania Kelvin John Ametajwa kwenye Orodha ya Wachezaji Bora 60 Duniani Wenye Umri Mdogo

Orodha hiyo imetolewa na Gazeti Kubwa la The Guardian la Uingereza

Kelvin John (17), mchezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana maarufu kama Serengeti Boys ametajwa katika orodha ya gazeti kubwa duniani la The Guardian la Uingereza kama mmoja miongoni mwa wachezaji 60 wenye umri mdogo bora duniani kwa mwaka 2020.

 

Kelvin, akijulikana pia kama “Tanzanian Mbappé” alifanya vizuri kwenye mashindano ya mataifa Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17) mwaka 2019 hadi kupelekea aliyekuwa kocha wa Taifa Stars Emanuel Amunike, kumuita kwenye kikosi cha timu ya taifa.

 

Kwasasa, Kelvin yupo kwenye shule ya michezo ya Brooke House College Football Academy nchini Uingereza.