
Picha ya kusikitisha inaonyesha mtalii
akipanda hadi ukingoni mwa Maporomoko ya Victoria ya Zimbabwe - muda mfupi tu
kabla ya kuanguka na kufariki kutoka urefu wa futi 350 (zaidi ya mita 100), vyombo vya habari
vya ndani vimeripoti.
Marehemu, Roy George Tinashe Dikinyay (40),
alikuwa akifanya zamu na familia yake kupiga picha kutoka eneo la juu la
maporomoko makubwa ya maji wakati ndipo alipoteleza na kuanguka, mashuhuda
waliiambia gazeti la Zimbabwe Newsday.
"Tulishtushwa na mayowe ya mwanamke huyo
akituambia kwamba alikuwa ameteleza na kuanguka," mmoja wa mashuhuda
aliliambia gazeti hilo. Dikinya ambaye alikuwa amevaa viatu huku
ameshikilia vitu kadhaa katika mkono wake wa kushoto kwenye picha hiyo.
"Kwa sababu ya mvua na ukungu,
hatukuweza kumtafuta baada ya tukio hilo," shahidi huyo alisema. Waokoaji
na Mamlaka ya Hifadhi za Kitaifa na Wanyamapori nchini Zimbabwe walipata sehemu
za mwili zimenaswa chini ya korongo, ambalo lina urefu wa futi 350, jarida la Chronicle limesema.
Sehemu za mwili "zimenaswa kati ya
miamba," msemaji wa mamlaka hiyo, Tinashe Farawo, aliliambia jarida hilo.
"Hatujaweza kumtambua vyema kutokana na eneo ambalo mwili wake umenaswa,
lakini tuna hakika kuwa ni mwili wake," alisema.
"Hivi sasa tunazungumza na wataalamu wengine wa usalama pamoja na jeshi kujaribu kupata njia
za kuuchukua mwili," alisema, na tuna njia moja ambayo ni kujaribu kutumia
helikopta ya jeshi.
Waziri wa Utalii na Mazingira, Mangaliso Ndlovu alituma "salamu za pole" kwa familia ya mtalii huyo ambaye anatoka mji mkuu wa Zimbabwe Harare, zaidi ya maili 400 kutoka kwa maporomoko hayo, gazeti la The Herald, Zimbabwe lilieleza.
Hatujaweza kumtambua vyema kutokana na eneo ambalo mwili wake umenaswa, lakini tuna hakika kuwa ni mwili wake
- Tinashe Farawo
"Matukio kama haya huwa ni machache,
yanasikitishana na ni bahati mbaya kushuhudiwa katika maporomoko makubwa ya
Victoria," Ndlovu alisema, huku akiahidi "tahadhari zote muhimu
zitachukuliwa ilikujilinda dhidi ya tukio baya kama hilo." Ni moja kati ya
matukio machache ya hivi karibuni yanayohusisha watu kuanguka huku wakichukua
picha kutoka kwenye maeneo hatari. Wiki chache zilizopita, mwanaume mmoja wa Brazil alikufa baada ya kuanguka
kutoka kwenye maporomoko ya maji akichukua “selfie”.
Leave a comment