Maisha

Mitego 4 ya Kisaikolojia Inayotumiwa na 'Supermarkets' Kukurubuni Ufanye Manununuzi

Sio bahati mbaya kukuta karibu Supermarket zote huwa na muonekano unaofanana kwa ndani na huwa na wafanyakazi ambao wapo tayari kukuzungusha ndani ya duka kuhakikisha unapata unachohitaji bila kukata tamaa

Umewahi kujiuliza kwanini takribani supermarket zote zina mpangilio unaofanana? Hii sio bahati mbaya. Ni matokeo ya majaribio ya ujanja wa kisaikolojia katika jitihada za kumrubuni mteja ili afanye manunuzi.

Baadhi ya mitego wanayotumia ni;

1.Hukuchanganya na Wingi wa Vitu

Wanauchumi na viongozi wa biashara wanatuambia kuwa chaguo zaidi moja ni sahihi. Lakini ukweli ni kwamba kama ungekuwa na uwezo wa kupata kila unachokitaka ulimwenguni basi ungekuwa na wakati mgumu.

Kwa nini? Kwa sababu, kulingana na tafiti, machaguo yasiyo na kikomo hufungua mlango wa majuto, mashaka na kutoridhika

Wakati tunakabiliwa na chaguzi nyingi sana, hatuwezi kushughulikia. Kwa hivyo tunaishia kunyakua chochote, au kununua zaidi na kulipa zaidi.

Unakuta ‘Supermarket’ ndogo ina wastani wa vitu 6000 vya kuchagua hivyo nafasi ya kuchanganyikiwa ni kubwa kama huwezi kufanya maamuzi sahihi.

2. Akili Yako Hulemewa

‘Supermaket’ hutaka kuvutia hisia za kila mtu anayeingia kufanya manunuzi. Mfano:

- Huweka Taa kali,rangi zinazong’aa

Bidhaa mpya zikionekana wazi na vioo vinavyokuwezesha kuona watu wakiwa kazini- waokaji, wauzaji ‘icecream’ kuvutia macho yako.

- Bidhaa zote zinaonyeshwa ili zikuvutie na uweze kuzigusa.

-Maua safi hunukia puani mwako pindi unapokanyaga mlango wa kuingilia. Keki safi za kuoka, harufu ya icecream vyote hivi hulenga kumvutia mteja.

-Sampuli za bure hupatikana kila wakati,na zinahimizwa na wafanyakazi ili uangukie katika mtego wa ladha.

3. Hucheza na Bei

Hii pia ni mbinu ambayo utumika kumrubuni mteja pindi aingiapo supermarket. Mfano unaweza kuwekewa bei ya awali na sasa ambapo mara nyingi huwa ni punguzo hivyo ukakurupuka kununua kuogopa bei ya juu pindi utakaporejea tena.

4. Hukutembeza Ndani ya Duka

Sio bahati mbaya kwamba karibu Supermarket zote huwa na muonekano unaofanana kwa ndani na huwa na wafanyakazi ambao wapo tayari kukuzungusha ndani ya duka kuhakikisha unapata unachohitaji bila kukata tamaa. Mpangilio huo ni sehemu ya mikakati ya kisasa ya kisaikolojia ya kukushawishi kutumia pesa zaidi.

Kumbuka sio lazima uangukie kwenye mitego ambayo Supermarkets hufanya. Unaweza kupata kile unachotaka kutoka duka na ukaepuka ujanja wa kisaikolojia ambao umeundwa kumaliza pesa zako kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo kufanya manunuzi huku ukizingatia bajeti uliyokuwa umeiandikia, kufanya m,anunuzi kwa msimu n.k