
Moja ya meli kubwa ya mizigo inayofahamika kama Ever Given Marine imekwama kwenye mfereji wa Suez na kusababisha msongamano wa meli katika moja wapo
ya njia zenye shughuli za biashara ulimwenguni.
Mfereji wa Suez ni moja wapo
ya njia muhimu za maji ulimwenguni na inaunganisha Bahari ya Shamu na njia za
usafirishaji kwenda Asia. Ina urefu wa km190, mita 24 kwenda chini na mita 205
kwa upana na inaweza kushughulikia meli kadhaa kubwa za makontena kwa siku.
Ever Given iliyo na urefu wa
mita 400 sawa na urefu wa viwanja vinne vya soka na upana wa mita 59 imeziba
njia za meli zingine ambazo zimekwama pande zote.
Meli hiyo iliyo na ukubwa wa
tani 200,000 iliundwa mwaka 2018 na ilikuwa ikiendeshwa na kampuni ya uchukuzi
ya Taiwan, Evergreen Marine ilikwama majini siku ya Jumanne
Evergreen Marine, imesema
meli hiyo "huenda ilikabiliwa ghafla na upepo mkali, ulioifanya kupoteza
mkondo… na kwa bahati mbaya kugonga chini na kukwama"
Ever Given ilikwama karibu na mwisho wa mfereji Jumanne baada ya kupoteza uelekeo kutokana na upepo mkali na dhoruba ya vumbi, Mamlaka ya Mfereji wa Suez ilisema.
Misri imesema imefungua njia
ya zamani kugeuza mkondo wa meli zingine ili kuzuia msongamano, huku kukiwa na
wasi wasi njia ya sasa itazibwa kwa siku kadhaa.
Tukio hilo tayari
limesababisha msongamano wa majini huku baadhi ya meli zikikosa njia ya kupita.
Boti kadhaa za kukokota zinafanya
kazi ya kuikomboa meli hiyo iliyozuia njia huku Wataalamu wakihimiza umakini
wakati wa oparesheni ya kuondoa Ever Given, ambayo inajumuisha kuondoa kiwango
kikubwa cha mchanga iliyozunguka sehemu iliyokwama meli hiyo, huenda ikachukua
siku kadhaa.
Tukio kama hilo limeshawahi
kutokea hapo awali ambapo mnamo mwaka wa 2017, meli ya Japani ilikwama lakini
ilirudishwa ndani ya masaa kadhaa. Mbali na mfereji huo, tukio kubwa zaidi
lilitokea karibu na bandari ya Ujerumani ya Hamburg mnamo 2016 wakati Meli
kubwa ya CSCL ilipokwama na kuhitaji maboti 12 kuikomboa zoezi lililochukua
takribani siku tano.
Leave a comment