Habari

Mapenzi ya Kukabana Koo Huenda Yakabatilishwa Nchini Uingereza

Kukaba koo pasi mauaji ni kosa kubwa ambalo limekuwa likilindwa na sheria zilizopo kama vile shambulio la kawaida na jaribio la mauaji

Kumkaba koo mpenzi wako wakati wa kufanya mapenzi inaweza kuwa kosa la jinai nchini Uingereza chini ya sheria mpya ya unyanyasaji wa majumbani.

Pendekezo la wanaharakati linakuja baada ya kuwepo kwa ushahidi wa kuridhisha kudhihirisha kuwa mmoja kati ya wahanga watano wa mauaji yanayotokana na unyanyasaji wa kingono amenyongwa na mwenza wao.

Kukaba kunaadhibiwa tu chini ya sheria ya kawaida ya shambulio, ambayo adhabu yake kubwa huwa haizidi miezi sita. Lakini vikundi vya kupinga unyanyasaji wa majumbani vimesema wahusika mara chache wanashtakiwa kwa sababu washtakiwa wanadai kwamba kukaba hufanyika kama sehemu ya makubaliano wakati wa kujamiina na kunaweza kuwa na ishara kidogo ya kuumia kimwili.

Wanaharakati wanaopinga kitendo hili wanadai kuwa kufanya kukaba kama shambulio la kawaida kunadhoofisha ukali wake na maumivu wanayoyapitia wahanga.

Ripoti hiyo inataja takwimu ya 2018 ambayo inanukuu kwamba karibu theluthi moja ya mauaji ya wanawake nchini Uingereza yalitokana na kukabwa au kukosa hewa ikilinganishwa na asilimia tatu ya mauaji ya wanaume. Vitendo hivyo vya kingono ni sababu ya pili ya vifo vya wanawake vinavyotokana na unyanyasaji majumbani ikiongozwa na mauaji ya kuchomana visu.

Kamishna mwakilishi wa unyanyasaji wa majumbani Nicole Jacobs na Kamishna mwakilishi wa wahanga, Dame Vera Baird wamesema wataunga mkono marekebisho hayo ambayo yatawasilishwa na kamishna muwakilishi wa wahanga wa zamani, Baroness Newlove katika Nyumba ya juu ambayo itageuza unyongaji pasi mauaji kuwa kosa moja.

 Ripoti hiyo ya habari pia inamtaja Mkurugenzi wa Kituo kinachoshughulikia matukio ya unyanyasaji wa kingono cha Mtakatifu Mary jijini Manchester,Dk Catherine White, akisema kwamba moja ya tano ya wanawake ambao walibakwa na wenzi wao walidai kuwa walikabwa walikabwa. Dkt White alisema zaidi kuwa sheria iliyopo haiendani na hali ya sasa na mageuzi yataleta uelewa na kustakiwa kwa wote watakaohusika na kitendo hicho.

 Dame Vera na Bi Jacobs wamepangwa kukutana na Katibu wa Sheria Robert Buckland siku ya alhamisi ili kujadili mapendekezo yao. Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na wao, wawili hao walisema ukabaji usiohusisha mauaji ni ‘tendo la hatari kabisa '. Walisema kwamba wahanga na manusura walikuwa wakifelishwa na sheria iliyopo na kuongeza, “ unyongaji wa namna hiyo umekuwa haupewi kipaumbele kama mashtaka mengine nchini Uingereza”.

Msemaji wa Wizara ya Sheria alisema, “kukaba koo pasi mauaji ni kosa kubwa ambalo limekuwa likilindwa na sheria  zilizopo kama vile shambulio la kawaida na jaribio la mauaji.”