Habari

Mafunzo ya JKT kwa Kujitolea Yasitishwa

Hata hivyo, taarifa hiyo haijatoa sababu ya maamuzi ya kusitishwa kwa mafunzo hayo

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetoa taarifa ya kusitisha mafunzo ya kujitolea kwa mwaka 2020/2021 yaliyokuwa yaanze hivi karibuni katika makambi mbalimbali nchini.

Kutokana na kusitishwa kwa mafunzo hayo, JKT linawataka vijana wote ambao walichaguliwa na kuripoti makambini kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa kujitolea, warejee majumbani kwao, na wale ambao walikuwa bado hawajaripoti wasiende kuripoti katika makambi waliyopangiwa mpaka hapo itakapotangazwa tena.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya JKT iliyotolewa Januari 19, 2021 mafunzo hayo yamesitishwa kwa muda usiojulikana. Hata hivyo, taarifa hiyo haijatoa sababu ya maamuzi ya kusitishwa kwa mafunzo hayo.