Duniani

Kwanini Philip aliitwa Mwanamfalme na Siyo Mfalme?

Mwanamfalme Philip, ambaye ni Mwanamfalme wa zamani wa Denmark na Ugiriki hakuwa kwenye orodha ya watu wanaostahili kukalia kiti cha Ufalme Uingereza

Mwanamfalme Philip, Mtawala wa Edinburgh alifariki Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 99.

Philip alimuoa Malkia Elizabeth II miaka mitano kabla ya kuwa Malkia mara baada ya Malkia kukabidhiwa taji hilo, Philip hakupewa cheo cha Ufalme na badala yake alifanywa kuwa Mwanamfalme

Ni nini Sababu?

Mwanamfalme Philip, ambaye ni Mwanamfalme wa zamani wa Denmark na Ugiriki hakuwa kwenye orodha ya watu wanaostahili kukalia kiti cha Ufalme Uingereza.

Philip alilazimika kuachia cheo cha Mwanamfalme wa Denmark na Ugiriki mara baada kumuoa Malkia Elizabeth II na kuwa mtawala wa Edinburgh

Philip alimuoa Malkia Elizabeth II mnamo 1947 na alikua malkia mnamo 1952 baada ya kifo cha baba yake, Mfalme George VI. Baadaye alimpa mumewe cheo cha “Mwanamfalme”

Cheo hiki hakikuwa kidogo kwa Philip hakutakiwa kuitwa mfalme wala Mwanamfalme. Cheo chake kilikuwa Duke wa Edinburgh hadi Februari 22, 1957 wakati ikulu ilipotoa taarifa kuwa Mtawala wa Edinburgh atakuwa Mwanamfalme wa Uingereza:

Kwa hiyo, malkia alimpa mumewe cheo cha ‘Mwanamfalme’ wakati alipotwaa taji na Siyo Mfalme, Kwanini?

Mwanamke anayeolewa na Mfalme anaweza kuitwa Malkia, lakini kwa wanaume ambao wanaoa Malkia kuna sheria tofauti hawawezi kutumia jina la mfalme kulingana na BBC News sababu ni kuwa cheo hicho kinatajwa kuwa mahususi kwa wanaume wanaorithi kiti hicho.

Hivyo, mtoto wa kwanza wa wenzi hao kama Charles, Mwanamfalme na mtawala wa Wales atapokea jina la mfalme pindi atakapochukua wadhifa huo.