Habari

Kitendawili Cha Covid-19 Tanzania Majibu Yaja

Serikali ya Tanzania imekuwa ikipambana na ugonjwa wa Covid 19 kitofauti ukilinganisha na nchi nyingine duniani kote huku ikipuuza kufuata masharti ya Shirika la Afya Duniani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema ataunda kamati itakayofanya uchunguzi kitaalamu na kumshauri juu ya kitendawili cha uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 nchini Tanzania.

 

Samia amesema hayo leo Aprili 6, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya uapisho wa uteuzi uliofanyika hapo jana.

 

“Kuhusu suala la Covid-19 nafikiria niunde kamati ya wataalamu waliangalie kwa upana wake kitaalamu halafu watushauri serikali. Halifai kulinyamazia aidha kulikataa au kulikubali bila kufanya tafiti za kitaalamu.” Amesema Samia Suluhu Hassan.

 

Wizara ya afya nchini Tanzania bado haijathibitisha taarifa za uwepo wa wagonjwa au vifo vinavyotokana na virusi vya corona huku Aprili mwaka jana ikiwa ni mara ya mwisho kutolewa kwa taarifa za mwenendo wa maambukizi ya gonjwa hilo.