
Katika mazingira ya kawaida, picha
inayomwonesha baba akinyonya maziwa ya binti yake inaweza kuwa ya kuchukiza kwa
sababu inaonesha kukosa maadili. Lakini mtazamo wako unaweza kubadilika baada
ya kusoma hadithi hii ya kusikitisha nyuma ya michoro hii yenye mkanganyiko wa
kihisia.
Michoro hii imetokana na hadithi iliyopewa
jina Ufadhili
wa Kirumi. Hadithi hii inamhusu baba aliyeitwa Pero na binti yake
aliyeitwa Cimon. Pero alihukumiwa kwenda jela na adhabu ya kifo kwa njaa
kutokana na kosa la kuiba mkate wakati wa utawala wa Mfalme Louis wa Kumi na Nne wa
Ufaransa.
Kama sehemu ya utekelezaji wa adhabu yake,
Pero hakuruhusiwa kuonana na mtu yeyote kwa kipindi chote atakapokuwa jela hadi
pale atakapokamilisha adhabu yake, yaani atakapokufa, isipokuwa binti yake. Na
wakati wote Cimon alipoenda jela, alipaswa kukaguliwa barabara kuhakikisha
hakuingia na chakula chochote.
Lakini kwa hali ya mshangao, Pero aliendelea
kuishi jela kwa muda wa miezi minne! Ndipo walinzi walipoanza kumtilia mashaka
na kuanza kuchunguza mienendo ya Cimon kila alipoingia jela. Baada ya muda,
walimkamata Pedro akiwa ananyonya maziwa ya binti yake! Cimon alikamatwa na
kupandishwa kizimbani, lakini kitendo hicho kiliwashawishi mahakimu kumwonea
huruma Pero na hatimaye akaachiwa huru.
Wasanii wengi walioishi karne ya 17 na 18 wamefanikiwa kusimulia kisa hicho kwa njia ya michoro, wakiwamo Peter Paul Rubens, Caravaggio, Hans Sebald Beham na Rembrandt Peale.
Mchoro wa Peter Paul Rubens
Sanamu inayoonesha kisa hicho pia imechongwa katika jengo moja nchini Ubelgiji. Sanamu hiyo inayoitwa "mammeloker" inamaanisha "myonya maziwa" kwa lugha ya Kiholanzi. Jengo hilo liliwahi kusemekana kuwa ni lango la kuingilia katika gereza kuu la mji.