Habari

Kampuni ya Boeing Yachapwa Faini ya Tsh. Trilioni 5.7

Kampuni ya ndege ya Boeing ilificha taarifa za Kiusalama za Ndege za 737 Max ambayo ilipata ajali na kuua watu 346 wakiwemo wafanyakazi waliokuwemo ndani

Boeing italipa faini ya Dola bilioni 2.5 ambayo ni takriban Tsh. Trilioni 5.7 kwa kosa la kuficha Taarifa za Kiusalama za Ndege za 737 Max ambayo ilipata ajali na kuua watu 346. Kampuni ya anga ya Boeing imetozwa faini ya Dola za Kimarekani bilioni 2.5 ambayo ni takribani Tsh. Trilioni 5.7 kufuatia ajali mbili zilisababishwa na ndege hizo.  Wizara ya sheria ya Marekani imesema ufumbuzi uliofikiwa unahusu adhabu ya faini ya dola milioni 243.6, malipo ya dola bilioni 1.77 kwa wateja wa kampuni ya Boeing 737 na kuanzisha mfuko wa dola milioni 500 kwa ajili ya fidia kwa warithi, ndugu na jamaa wa watu waliokufa katika ajali.Ajali mbili za ndege za Boeing 737 zilitokea nchini Indonesia mnamo mwaka 2018 na nchini Ethipia mnamo mwaka 2019 ambapo kwa jumla watu 346 walikufa.

Ajali mbili za ndege za Boeing 737 Max zilizotokea nchini Indonesia mnamo 2018 na nchini Ethiopia mnamo 2019  ambapo kwa ujumla idadi ya watu wakiwepo wafanyakazi waliokuwa ndani  waliaga dunia.

Baada ya ajali hatua stahiki zilichukuliwa zikihusisha uchunguzi kadhaa ulioigharimu kampuni hiyo  karibu Dola za Kimarekani bilioni 20 .Safari za Ndege zote za 737 Max zilisitishwa mpaka pale serikali ya Marekani ilipotoa ruhusa  kwa Boeing kuanza kuzirusha  tena mnamo Novemba ambapo ndege zilianza safari zake rasmi pindi ilipotimu Disemba mwaka jana. Boeing ilihitajika kuboresha programu, mifumo na mafunzo yake kabla ya kubeba abiria kwenye ndege.

Mkurugenzi wa mamlaka ya anga nchini Marekani (US Federal Aviation Administration (FAA) Chief), Steve Dickson alisema mwaka jana idara hiyo "imefanya kila linalowezekana” kuhakikisha aina hizi za ajali hazitokei tena. Alisema alikuwa na imani kwa asilimia 100 katika usalama wa ndege hiyo.

Taarifa zilizofichwa zilikuwa ni kuhusu kubadili Mfumo wa MCAS ambao ulifanya Rubani akose baadhi ya taarifa kuhusu Mfumo huo wa Uendeshaji ambapo walikuwa wakilazimisha vinginevyo kwa kutojua.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Boeing, David Calhoun alisema katika makubaliano hayo "yanakubali kwamba walienda kinyume na maadili na matarajio".