Habari

Joe Biden Rasmi White House

Kiapo cha Biden kilisimamiwa na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu, John Roberts mbele ya viongozi wa mabunge kutoka pande zote na marais wa zamani wakiwemo Barack Obama, Bill Clinton na George W Bush

Joe Biden aapishwa rasmi kuwa rais wa 46 Marekani ikiwa ni siku 72 zimepita tangu atangazwe kuwa mshindi wa kiti cha urais mnamo Novemba 7.

Kiapo cha  Biden kilisimamiwa na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu, John Roberts mbele ya viongozi wa mabunge kutoka pande zote na marais wa zamani wakiwemo Barack Obama, Bill Clinton na George W Bush  huku   Trump ambaye alikataa kushiriki tangu awali akiwa Florida ambapo alisafiri  asubuhi ya jumatano.

Joe Biden alishinda kiti cha urais kupitia tiketi ya chama cha Democratic huku mpinzani wake mkubwa akiwa ni aliyekuwa Rais wa nchi hiyo mwaka 2016-2021 chama, Republican.

Biden aliondoka mjini kwake Deleware kuelekea Washngton masaa machache kabla ya Uapisho huku akitoa hotuba iliyoibua hisia  na kumtoa machozi huku akisema

"Samaheni hisia zangu, lakini nitakapokufa, Delaware itaandikwa moyoni mwangu," Biden alisema.