
Kuongezeka kwa mitandao ya kijamii kunamaanisha kuwa watu wameunganishwa zaidi kuliko vile tulivyowahi kuwa historia ya nyuma. Lakini utegemezi wetu kwenye mitandao ya kijamii unaweza kuwa na athari mbaya kwa afya yetu ya akili.
Binadamu ni viumbe wa kijamii. Tunahitaji kushirikiana na wengine ili tufanikiwe maishani, na nguvu ya uhusiano wetu ina athari kubwa kwa afya yetu ya akili na furaha. Kuwa na uhusiano wa kijamii na wengine kunaweza kupunguza mafadhaiko, wasiwasi, kuongeza kujithamini, kutoa faraja na furaha, kuzuia upweke, na hata kuongeza miaka kwenye maisha yako. Kwa upande mwingine, kukosa mahusiano mazuri na jamii kunaweza kusababisha hatari kubwa kwa afya yako ya akilina hisia.
Katika ulimwengu wa leo, wengi wetu tunategemea majukwaa ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Snapchat, YouTube, na Instagram kujenga mahusiano na kuungana. Wakati kila mtandao una faida zake, ni muhimu kukumbuka kuwa mitandao ya kijamii haiwezi kuwa mbadala wa makutano ya kibinadamu. Inahitaji mawasiliano ya ana kwa ana na wengine ili kuchochea homoni ambazo hupunguza mafadhaiko na kukufanya ujisikie furaha na afya njema.
Badala ya teknolojia ambayo imeundwa kuwaleta watu karibu kuwafanya watu wawe na furaha, kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kunaweza kukufanya mtu ukapata hisia ya huzuni, upweke, kutengwa, kutoridhika, kuchanganyikiwa hali ambayo inaelezea athari katika afya yako ya akili. Kwa watu wengi, ukiangalia kwa uangalifu ukurasa wako wa mtandao wa kijamii waTwitter kabla tu ya kulala inaweza kuchangia katika hali duni ya kulala. Hivyo ni vizuri kama utajenga uwiano mzuri kati ya mitandao ya kijamii na maisha binafsi .
Athari chanya za kutumia
mitandao ya kijamii:
Wakati mwingiliano wa kawaida kwenye
mitandao ya kijamii hauna faida ya kisaikolojia sawa na mawasiliano ya
ana kwa ana, bado kuna athari chanya za kutumia mitandao ya kijamii.
Mitandao ya kijamii
hukuwezesha:
a)Kuwasiliana na kuendeleza mahusiano
na familia pamoja na marafiki ulimwenguni kote.
b) Kujenga urafiki na watu
wapya; ambao masahi yenu yanakuwa yanaendana.
c)kuongeza uelewa juu ya
maswala muhimu.
d)Tafuta au kutoa msaada wakati
wa nyakati ngumu.
e) Njia ya kujipatia kipato kupitia biashara mbalimbali unazoweza kuzifanya mtandaoni.
f) Sehemu ya kujifunza mambo
Athari hasi za kutumia mitandao ya kijamii
Soma kwenye orodha ya
athari hasi za mitandao ya kijamii. Ukiiona yeyote ambayo unaweza kuihusianisha
na maisha yako binafsi basi inaweza kuwa ni ishara inayokutaka kupunguza
matumizi yako au hata kuacha kutumia mitandao ya kijamii kabisa.
a) Mfadhaiko na Wasiwasi
Je, unatumia saa kadhaa kwa siku
kuvinjari kupitia mitandao ya kijamii? Kutumia muda mrefu sana kwenye tovuti za
mitandao ya kijamii kunaweza kuathiri hisia zako. Watumiaji sugu wana uwezekano
mkubwa wa kuathiri afya zao za akili. Haichukui muda mrefu
kufikiria sana kujua ni kwanini. Watumiaji wa mitandao ya kijamii hukuonesha sehemu bora
zaidi walizochagua kwenye maisha yao, ambapo tatizo hutokea pale utakapolinganisha na sehemu hasi katika maisha yako. Kujilinganisha na watu
wengine ni njia ya mojawapo ya kukuletea mfadhaiko, na mitandao ya kijamii
imefanya hii iwe rahisi zaidi.
Kwa hivyo unawezaje kutumia
mitandao ya kijamii bila kusumbua saikolojia yako? Ukigeukia tafiti nyingi na
akili yako ya kuzaliwa, muda uliopendekezwa kutumia kwenye mitandao ya kijamii
ni nusu saa kwa siku. Kama yalivyo mambo mengine katika maisha, hili suala la matumizi ya mitandao ya kijamii linahitaji kiasi.
b)Unyanyasaji mtandaoni
Kabla ya mitandao ya kijamii,
uonevu ilikuwa jambo ambalo lilikuwa linawezekana tu kufanywa ana kwa ana.
Walakini, sasa watu wanaweza kuwaonea wengine mtandaoni wazi wazi au hata
bila kujulikana. Leo kila mtu anajua unyanyasaji wa mtandao ni
nini, na wengi wetu tumeona vile hufanywa .
Wakati mitandao ya kijamii inafanya
iwe rahisi kukutana na watu wapya na kupata marafiki, pia imewezesha watu wakatili
kuwanyanyasa wengine kirahisi zaidi. Wafanyaji wa uonevu wanaweza kutumia
kurasa bandia mitandaoni ili kutekeleza dhamira yao mbovu . Mashambulio
haya mtandaoni mara nyingi husababisha athari ya afya ya akili kwa mtendwa hata
kusababisha watu kujiua katika visa vingine. Na si kwa watoto tu, watu wazima
wanaweza kuwa wahanga pia wa unyanyasaji mtandaoni.
c) Hofu ya Kukosa
Ni jambo ambalo lilizaliwa karibu
wakati huo huo wa kukua kwa mitandao ya kijamii. Haishangazi, ni moja wapo ya
athari mbaya sana za mitandao ya kijamii kwenye jamii.
Hofu ya kukosa ni aina ya wasiwasi
unayopata wakati unaogopa kukosa mambo mazuri yanayofanywa na mtu mwingine. Kwa
mfano, unaweza kukagua ujumbe wako kila mara ili uone ikiwa kuna mtu
amekualika, au kuangalia kila wakati ni nani amekuomba urafiki au ame "like”
picha yako au nani kushinda instagram siku nzima ili kuhakikisha kuwa hakuna
mtu anayefanya kitu kizuri kukushinda.
Kwa kuongezeka kwa matumizi ya
mtandao wa kijamii, ni rahisi kutokutosheka na maisha yako binafsi na hii ndiyo
huzalisha hofu ya kukosa.
d) Matarajio yasiyo halisi
Kama watu wengi labda wanajua kwa
sasa, media ya kijamii huunda matarajio yasiyo ya kweli katika maisha na
urafiki kwenye akili zetu. kurasa nyingi za mitandao ya kijamii zina ukosefu
mkubwa wa uhalisi. Watu hutumia Snapchat kuchapisha vituko vyao vya kusisimua,
kuchapisha juu na jinsi wanavyopenda na wapenzi wao kwenye Facebook, na
kupakia kurasa zao za Instagram na picha bandia.Wakti hauna njia ya kujua kama
mambo hayo yote ni ukweli unaweza kukuta mtu huyo ana deni kubwa au ana
migogoro na mwenza wake an wakati mwingine anachapisha picha zake mtandaoni
kutafuta “likes” ambazo humfanya ajione bora zaidi machoni mwa watu. Njia moja
rahisi kutoka kwa fujo hii ni kwa kila mtu kuacha kuongopa kwenye mitandao ya
kijamii jambo ambalo haliwezi kutokea hivi karibuni kwani watu wengi huingiza
mamilioni katika Instagram na youtube kwa kusema uongo.
e) Huathiri Usingizi wako
Juu ya kuongeza visa vya wasiwasi na
mfadhaiko, kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kunaweza kuathiri utaratibu
wako wa kulala. Tafiti nyingi zimeonesha kuwa kuongezeka kwa utumiaji wa
mitandao ya kijamii kuna athari mbaya katika kulala kwako.Ikiwa utaratibu
wako wa kulala umevurugika jaribu kupunguza kiwango cha wakati unaovinjari
kwenye mitandao ya kijamii.
Hii ni kesi hasa wakati wa kutumia
simu yako kitandani usiku. Ni rahisi sana kusema utatumia dakika tano kupitia
ukurasa wako wa facebook na kujikuta unaperuzi saa zima twitter kwenye kurasa
ambazo hazina hata maana.
f) Kutoridhishwa na maisha au
muonekano wako binafsi
Hata ikiwa unajua kuwa picha
unazotazama kwenye mitandao ya kijamii sio halisi, bado zinaweza kukufanya
ujisikie kutokutosheka juu ya jinsi unavyoonekana au kinachoendelea katika
maisha yako mwenyewe. Ilhali tunajua watu huchapisha yale mazuri tu katika
kurasa zao za mitandao lakini bado tumekuwa tukiwaonea wivu na kutamani maisha
yao pindi tunapokuwa tunapita katika kurasa za mitandao yao ya kijamii.
Kila mtu ni tofauti na hakuna
kiasi cha muda unachotumia kwenye mitandao ya kijamii, au idadi ya maudhui
unayochapisha mtandaoni yataonesha kuwa matumizi yako yanaathiri
afya yako ya akili. Badala yake tunaangalia ni kwa jinsi gani muda unaotumia
kwenye mtandao wa kijamii unaathiri muonekano wako, maisha yako na namna unavyojihusisha na mitandao ya kijamii.
Kwa mfano, matumizi yako ya mitandao ya kijamii yanaweza kuwa na shida ikiwa inakusababisha kupuuza uhusiano wa ana kwa ana, kuathiri utendaji wako wa kazi au mahuidhurio shuleni, au kukuacha ukiwa na wivu, hasira, au mfadhahiko. Vivyo hivyo, ikiwa unahamasishwa kutumia media ya kijamii kwa sababu tu ya upweke, au unataka kuchapisha kitu ili kuwafanya wengine waone wivu au wakasirike, basi itakuwa ni wakati muafaka wa kutathmini tabia zako katika mitandao ya kijamii.
Viashiria ambavyo huonesha
kuwa mitandao ya kijamii inaweza kuathiri afya yako ya akili ni pamoja na:
#1: Kutumia wakati
mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuliko na marafiki zako kwenye ulimwengu
halisi: Kutumia mitandao ya kijamii imekuwa mbadala ya muingiliano wako wa
kijamii nje ya mtandao. Hata ikiwa uko nje na marafiki, bado unahisi uhitaji wa
kuangalia kila kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii.
#2: Kujilinganisha
na wengine kwenye mitandao ya kijamii.
#3: Kuteteleshwa na
Unyanyasaji wa kimtandao .
#4: Athari katika
utendaji wa kazi au uwajibikaji shuleni. Unahisi shinikizo la kuchapisha picha
zako mtandaoni, kupata “likes” kujibu maoni kwenye machapisho yako, au
kujibu haraka na kwa shauku kwa machapisho ya marafiki.
#5: Kutokuwa
na wakati wa kujitafakari. Kila wakati wa ziada unaoupata unatumia kujihusisha
na mitandao ya kijamii ambayo hukuacha na muda mchache wa kujifanyia tafakari.
#6: Kujihusisha na
tabia hatarishi ili upate “likes”, Unacheza mizaha ya hatari, unachapisha vitu
vya aibu, unanyanyasa wengine mitandaoni au unatumia simu wakati ukiwa
unaendesha.
#7: Kuvuruga
utaratibu wa kulala; Je! Unachunguza mitandao ya kijamii kama jambo la mwisho
kufanya usiku , kitu cha kwanza asubuhi, au hata unapoamka usiku? Mwanga kutoka
kwa simu na vifaa vingine inaweza kuvuruga usingizi wako, ambayo inaweza kuwa
na athari kubwa kwa afya yako ya akili
#8: Dalili za kuongezeka kwa wasiwasi au msongo wa
mawazo. Badala ya kusaidia kupunguza hisia hasi na kuongeza furaha yako,
unahisi wasiwasi zaidi, mfadhaiko, au upweke baada ya kutumia media ya kijamii.
Jinsi ya Kuepukana
na Athari hizi
Kama ilivyokuwa kila kitu kina mazuri
na mabaya yake vivyo hivyo mitandao ya kijamii ina mazuri na mabaya yake.
Tumejadili athari baadhi ya athari hasi za mitandao ya kijamii kwa watu wengi,
lakini wewe ndiye unayepaswa kuamua ni jinsi gani utumie mitandao kwa namna
ambayo haitokuletea madhara.
Ukigundua kuwa mitandao ya kijamii ina athari mbaya kwenye maisha yako, acha. Lakini, ikiwa unaamua kutumia, tumia vidokezo vyetu kupoteza muda mdogo kwenye mitandao ya kijamii kudumisha furaha yako kwa njia nzuri.
Leave a comment