Habari

Fahamu Baraza Jipya la Mawaziri liloteuliwa na Rais Magufuli leo, Kigwangalla Nje

Rais Magufuli pia ameteua Manaibu Waziri 23 na Wabunge wawili ambao amewapangia majukumu ya kuwa Mawaziri

Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 ambayo Dkt. John Pombe Magufuli alitangazwa kuwa mshindi kwa 84%, Rais ameendelea kuunda safu ya Serikali yake kwa mujibu wa Katiba.

Leo amefanya Uteuzi wa Mawaziri 21 na Manaibu Waziri 23 na Wabunge wawili ambao amewapangia majukumu ya kuwa Mawaziri. Pia, Rais Magufuli ameunda Wizara mpya ambayo haikuwepo awali, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias John Kwandika

Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika. 

Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Waziri wa Maji, Juma Aweeso

Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Vijana na Ulemavu, Jenista Mhagama

Waziri wa Afya, Jinsia Wazee na Watoto, Gwajima Dorothy

Waziri Ofisi ya Rais, Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba

Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Mashauri Ndaki

Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro

Waziri wa wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa

Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jaffo

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamuliro

Waziri wa Madini, Dotto Biteko

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mwambe Godfrey Idelphonce

Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene

Waziri wa Mazingira na Muungano, Ummy Mwalimu

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Faustine Ndugulile.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango


Naibu mawaziri

Wizara ya Viwanda na Biashara- Kigae Silaoneka

Wizara wa Ardhi- Angelina Mabula

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira- Patrobas Katambi

Wizara ya Mambo ya Ndani- Hamis Hamza Hamisi

Wizara ya Fedha- Mwanaida Ali Khamis

Wizara ya Elimu- Kipanga Juma Omar

Tamisemi- Dk Festo Ndugange

Wizara ya Nishati- Stephen Byabato

Menejimenti Utumishi wa Umma- John Ndejembi

Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Kundo Mathew

Wizara ya Mifugo- Pauline Gekul

Wizara ya Madini- Ndulane Kumba

Wizara ya Ujenzi- Godfrey Kasekenya

Ofisi ya Waziri Mkuu wenye ulemavu- Ummy Ndelinanga

Wizara ya Maji-  Maryprisca Mahundi

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo-  Abdallah Ulega

Ofisi ya Makamu wa Rais (muungano na mazingira)- Mwita Waitara

Wizara ya Mambo ya Nje-  William Olenasha

Wizara ya Maliasili na Utalii- Mary Masanja

Ofisi ya rais Tamisemi- David Silinde

Wizara ya Kilimo- Hussein Bashe

Wizara ya Afya- Dk Godwin Mollel

Wizara ya Katiba na Sheria- Pinda Mizengo

Katika Baraza hili jipya la Mawaziri, Mawaziri sita wa Baraza lililopita hawajateuliwa tena wamewekwa pembeni na Rais Magufuli, Mawaziri hao ni Hamis Kigwangalla (Maliasili na Utalii), Profesa Makame Mbarawa (Waziri wa Maji), Musa Azzan Zungu (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina (Uvuvi na Mifugo), Injinia Isaac Kamwele (Ujenzi na Uchukuzi), Japhet Hasunga (Kilimo).


Manaibu Waziri ambao hawajarudi ni Juliana Shonza (Habari, Sanaa na Michezo), Anthony Mavunde (Vijana), Injinia Stellah Manyanya (Viwanda na Biashara.

Endelea kufuatilia Serengeti Post kwa taarifa mbalimbali