Habari

Eric Omondi Alazimika Kuomba Msamaha Punde Baada ya Kutoka Mikononi mwa Polisi

Katika sasisho lake lilionekana katika akaunti yake ya Instagram, Omondi alisema kuwa alikuwa na mazungumzo marefu na Afisa Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu (KFCB) Kenya, Ezekiel Mutua na sasa anaunga mkono maoni yake kwamba "Wife Material sio lazima ipotoke ili ifanye mauzo."

Mchekeshaji, Eric Omondi amelazimika kuomba msamaha kwa umma masaa machache baada ya kuachiliwa kutoka chini ya ulinzi wa polisi kufuatia mashtaka yanayomkabili kutokana na onyesho lake la Wife Material.

Katika sasisho lake lilionekana katika akaunti yake ya Instagram, Omondi alisema kuwa alikuwa na mazungumzo marefu na Afisa Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu (KFCB) Kenya, Ezekiel Mutua na sasa anaunga mkono maoni yake kwamba "Wife Material sio lazima ipotoke ili ifanye mauzo."


mchekeshaji huyo aliongeza kuwa lengo la kipindi chake sio baya bali ni kuwaleta pamoja watu kutoka Afrika Mashariki na Afrika nzima kupitia burudani.

Mchekeshaji Eric Omondi na baadhi ya washiriki 15 wa onyesho la 'Wife Material' waliachiliwa Ijumaa kutoka mahabusu za Polisi jijini Nairobi.

Washiriki hao wa kipindi cha ‘Wife Material’ waliachiliwa kwa dhamana ya Ksh50,000 (157,455Tsh) huku wakitarajiwa kufika kortini Machi 18 ili kukabiliana na mashtaka ya kushiriki katika utengenezaji wa “kipindi kisicho na maadili”.

Katika taarifa, KFCB ilisema kuwa mcheshi huyo alikamatwa kwa kukiuka Sheria ya Filamu na maonyesho ya sura 222, ambayo inakataza utengenezaji na usambazaji wa filamu zisizoidhinishwa.

”Maafisa wa Ufuatiliaji wa Bodi ya Uainishaji wa Filamu Kenya wakishirikiana na Maafisa wa Polisi kutoka Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) leo mchana wamedai kuwa Eric Omondi amekamatwa kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Filamu na Maonyesho ya Sura 222 ya Sheria za Kenya kwa kutengeneza na kusambaza filamu ambayo haijaidhinishwa kwa jina “Wife Material.”,taarifa ya Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi Filamu nchini Kenya (KFCB), Dkt. Mutua ilisema.".