Habari

Dkt Mwigulu: Wafanyabiashara Pelekeni Fedha Benki Kodi Itatozwa tu.

Waziri ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango mara baada ya kukabidhiwa ofisi hiyo

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara wanaoficha fedha majumbani kuacha kufanya hivyo na badala yake wahifadhi benki kwa usalama zaidi na kuongeza mzunguko wa fedha kwani haziwezi kunyang’anywa na serikali.

Akizungumza na menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango baada ya kukabidhiwa ofisi hiyo amesema β€œKwa wale Wafanyabiashara ambao walishaanza kuona nikiweka hela yangu ikaonekana mtandaoni labda itachukuliwa yote, nitoe rai warudishe fedha kwenye Mabenki, zitaliwa mchwa huko na panya bila sababu, uchumi wa kisasa sio wa kuweka fedha kwenye boksi, kodi itatozwa tu.” Mwigulu Nchemba

Kauli hiyo imepokelewa kwa ukosoaji kutoka kwa wanasiasa na wadau wengine wa biashra, kwani imetolewa kama kitisho kwa wafanyabiashara badala ya kutumia lugha nzuri ya kuvutia wafanyabiashara katumia lugha ya vitisho.

@mwigulunchemba1 Unafikiri watu walipenda kuficha pesa ndani ?kwanza wanazo ? Kuna watu wako jela kwa miaka kwa kukutwa na sh milioni 2 tu.Serikali ilidhulumu watu fedha kwa njia mbalimbali,watu wakaogopa ata ku dream utajiri,mitaji imeanguka,confidence ya kuwekeza imepotea...


Mmh labda katiba ibadilike ije mpya ndiyo tutweka hela bank but kwa katiba hiyo hiyo iliyowaruhusu kupora hela zetu leo imegeua kisha kaingia Mwigulu iseme wekeni hatuchukui tena 😝😝😝😝😝😝😝 WANYONGE (IGNORANTS) wataweka ili mzikwapue vizuri. Badili katiba kwanza