
Dkt.Philipo
Isdor Mpango Ameapishwa kuwa Makamu wa Rais, hafla hiyo imefanyika leo tarehe
31/03/ 2021 Ikulu Chamwino, kufuatia Uteuzi wake ulifanywa jana tarehe
30/03/2021 ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa Makamu wa Rais. Mh Samia Suluhu
Hassan kuchukua nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama kisemavyo
kifungu cha 37 ibara ya (5) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada
ya kifo cha aliekuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli.
Dkt.Mpango
atashika uongozi huo kwa kipindi kilichosalia cha miaka minne (04) ili
kukamilisha Uongozi wa Awamu ya tano (05).
Akihutubia
baada ya kuapishwa Dkt.Mpango alisema
“na katika kutekeleza majukumu unayonituma hakika nitashirikiana na viongozi
wenzangu inavyopaswa lakini pia mihimili yote ya Dola” Dkt. Philipo Mpango
Dkt.
Mpango ambaye aliingia Bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2015 kama mbunge wa
kuteuliwa na Rais kati ya Wabunge kumi wanaoteuliwa na Rais, na Mwaka 2020
aliingia Bungeni kwa mara ya pili huku akiwakilisha Jimbo la Buhigwe mkoani
Kigoma.
Dkt.
Mpango alikuwa Waziri wa Wizara ya Fedha tangu mwaka 2015, mpaka hapo jana
ambapo uteuzi wake ulikoma baada ya kuteuliwa na kuthibitishwa na Bunge kwa
kura 363 sawa na asilimia 100 kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.
Leave a comment