
Mwanamziki nguli wa
Tanzania Diamond Platnumz kutoka lebo ya Wcb Leo Tarehe 01/4/2021 ametangaza
kuingia Mkataba wa kuwa Balozi wa Bidhaa za Kampuni ya Simu za mkononi ya Itel.
Akiandika kwenye kurasa
zake za Mtandao wake wa Twitter na Instagram Diamond amesema “Nina Furaha kuwajuza kuwa
sasa ni Balozi wa Bidhaa za Itel.”
Hivi karibuni Diamond
Platnumz amekuwa akiingia Mikataba na makampuni mbalimbali ya ndani na Nje ya
Tanzania kufanya matangazo yao ya Bidhaa
mbalimbali.
Diamond Platnumz anatajwa
kuwa msanii Mwenye dili nyingi za matangazo kutoka Tanzania huku fununu zikidai
kwamba yeye ndiye Msanii anaelipwa zaidi kwenye kufanya matangazo kutoka
Tanzania.
Leave a comment