
Uchovu wa pombe kama
ijulikanavyo na wengi "Hangover" humfanya mtu ajisikie uchovu baada
ya kunywa kiasi kikubwa cha pombe.
Unapokunywa, pombe
huingia kwenye damu yako.Hivyo kufanya mchanganyiko wa pombe na damu na kiasi cha pombe kikiwa
kingi kwenye ndipo unapoanza kuhisi ulevi. Pindi ukiacha kunywa, kiwango hicho
huanza kushuka na "hangover" huwa mbaya zaidi wakati kiwango hicho
kinarudi sifuri na maranyingine huweza kudumu hata kwa masaa 24.
Hali hii huvumilika
mara nyingi lakini wakati mwingine huwa mbaya kiasi kwamba mtu huweza
kulazwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Ukweli ni kwamba hangovers sio jambo la kufurahisha. Unaweza kuugua maumivu ya kichwa, kutetemeka, maumivu ya tumbo na kuishiwa nguvu kabisa. Kabla ya kufikiria dawa za kupunguza maumivu na chakula chenye mafuta, ukweli ni kwamba hakuna kinachoweza kuzuia au kutibu hangover tiba sahihi ni subira na muda kama utakunywa pombe kupita kiasi.
Hizi ni baadhi ya dhana potofu kuhusu "hangover":
Dhana #1:
Pombe kali kabla ya bia
Katika maisha yako ya
ulevi unaweza ukawa umesikia msemo huu lakini ukweli ni kwamba msemo huu hauna
ukweli wowote .
Ni
kiwango cha pombe unachokunywa na sio mpangilio wa vinywaji vyako ambacho
ndicho muhimu zaidi. Mfano milimita 355 za bia, milimita 148 za mvinyo na
milimita 44 za pombe kalizina kiwango sawa cha pombe hivyo
usidanganyike na saizi ya kinywaji chako.
Dhana #2: Shtua pombe
kidogo baada ya kuamka
Kuongeza pombe baada
ya kuamka haisaidii kitu zaidi ya kuongeza muda wa kuuguza Uchovu wa pombe.
Ukweli ni kwamba pombe
itakufanya uzidi kukaukiwa maji mwilini ukizingatia
kiasi cha pombe kinakuwa bado kinazunguka ndani ya damu yako.
Dhana #3:
Lala Punde tu baada ya kulewa
Ukilewa pombe, kuamka
ni jambo ambalo huwa ni gumu sana siku inayofuata ingawa ndiyo njambo
bora unalopaswa kufanya. Pombe hutoka mwilini kwa njia mbili: kukojoa na
upumuaji. Kwa hivyo, inuka na utembee,kimbia na kunywa maji mengi.
Ukinywa pombe nyingi,
tulia kidogo kabla ya kulala kwani pombe huendelea kunyonya unapolala na
kuongeza kiwango cha pombe kwenye damu yako.
Dhana #4:
Walevi pekee hupata “hangover”
Sio lazima ulewe sana
ndo upate hangover asubuhi inayofuata. Vinywaji kadhaa tu vinaweza kusababisha
maumivu ya kichwa na dalili zingine za hangover kwa watu wengine. Kunywa maji au kinywaji kisicho na
kilevi wakati
unaendelea kunywa itakusaidia kusawazisha kiwango cha pombe mwilini.
Dhana #5:
Kunywa dawa za kupunguza Maumivu
Sio vizuri kunywa dawa
yoyote wakati wa kunywa pombe.
Dawa nyingine hasa
zile zilizo kemikali ya “acetaminophen” kama Tylenol kwani inaweza kusababisha
uharibifu wa ini lako ambalo linakuwa tayari limejaa pombe. Hivyo ni vyema
kusubiri hadi uamke asubuhi ndipo uchukue aina yoyote ya dawa ya maumivu.
Dhana #6:
Kujitapisha
Hii haina tija kabisa.
Watu wengi huamini njia hii ni sahii kwani hutapika kinywaji chochote
kinachokuwa mwilini lakini ukweli ni kwamba pombe huwa tayari imeengia ndani ya
damu hivyo kujitapisha ni kuendelea kujipunguzia maji mwilini bila kusahau
athari zinazotokana na kujilazimisha kutapika.
Dhana #7:
Kahawa ni Tiba
Ukweli ni kwamba kafeini iliyopo ndani ya kahawa huminya mishipa yako ya damu na huweza kufanya “hangover” yako kuwa mbaya zaidi. Baada ya usiku wa ulevi, ni bora kunywa maji na “energy drinks” ili kukabiliana na upungufu wa maji mwilini na kukupa nguvu hasa ukiwa umetapika.
Leave a comment