
Tuzo za Grammy za mwaka 2021 zinaahirishwa
hadi Machi 14 kwa sababu ya wasiwasi unaohusiana na janga la virusi vya corona.
Recording academy ambao ndiyo wanahusika
na ugawaji wa tuzo hizi wamethibitisha katika taarifa inayoeleza kwamba
inasogeza mbele tuzo hizo za kila mwaka kutoka Januari hadi Jumapili, Machi 14
kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya janga la corona hasa katika mji wa Los
Angeles, ambapo hafla hiyo itafanyika.
"Baada ya mazungumzo mazito na wataalam
wa afya, washereheshaji wetu na wasanii waliopangwa kushiriki, tunasogeza mbele
Tuzo za Grammy ambapo zitaenda kutangazwa Jumapili, Machi 14, 2021,"
taarifa ilisomeka.
"Hali mbaya ya COVID huko Los Angeles, na
huduma za hospitali kufurika, ICU kuzidiwa, na mwongozo mpya kutoka kwa
Serikali na serikali za mitaa zimetusaidia kuona kuwa uamuzi wetu wa kuahirisha
onyesho letu lilikuwa ni jambo sahihi,” taarifa hiyo ilisomeka.
“Hakuna kitu cha muhimu zaidi kuliko afya na usalama wa
wale waliopo katika jamii yetu ya muziki na mamia ya watu wanaofanya kazi bila
kuchoka kutayarisha onyesho hili. Tunataka kuwashukuru wasanii wote wenye
talanta, wafanyakazi, wauzaji wetu na hasa wasanii walioteuliwa kushiriki tuzo
hizi za mwaka huu kwa uelewa, uvumilivu na utayari wa kufanya kazi nasi hasa
tunapopitia nyakati hizi ngumu ambazo hazijawahi kutokea.”
Taarifa hiyo ilisainiwa na Harvey
Mason Jr., Mkurugenzi wa Recording Academy.
Tuzo hizo za Grammy zitafanyika Los Angeles
katika Kituo cha Staples, Kaunti ya Los Angeles, ambako ndio kitovu cha ugonjwa
huko California, ambako umezidi vifo 10,000 na imekuwa na asilimia 40 ya vifo .
Beyonce ndiye anayeongoza katika tuzo hizo mwaka huu akiwa na uteuzi katika
vitengo tisa.
Leave a comment