
CAF: Simba Mashabiki
10,000 tu kwa Mkapa
Shirikisho la
Mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limefikia uamuzi wa kuruhusu Klabu ya Mpira
ya Simba kutoka nchini Tanzania kuingiza uwanjani idadi ya mashabiki 10,000 tu wakati
itapokuwa inacheza na Klabu ya As Vita Club kutoka Congo lengo likiwa ni kudhibiti
hatari ya maambukizi ya corona.
Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 01/04/2021 Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema “Leo tumepata Habari njema kutoka CAF kuwa tumeruhusiwa kuingiza mashabiki 10,000 tu katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya As vita”
Simba itashuka
dimbani kuminyana na As Vita Club Jumamosi hii tarehe 03/04/2021, huku ikiwa na
faida ya kuongoza kundi lao, kucheza mchezo huo nyumbani, kushinda mechi ya
awali dhidi ya wapinzani wao na kucheza huku wakiwa na mashabiki.
Leave a comment