Habari

BrighterMonday Yazindua Kijitabu cha Mwongozo kwa Mwajiri (Employer Handbook)

BrighterMonday yazindua Kijitabu cha Mwongozo kwa Mwajiri (Employer Handbook) kinachoangazia namna bora za kufanya usimamizi wa rasilimali watu wakati wa majanga kama ya corona na hata baada ya hapo.

 

Katika kijitabu hicho, pamoja na masuala mengine kinaangazia hatua muhimu katika mchakato wa uajiri na ufanyaji maamuzi, mazingira na namna ya kufanya kazi kutokea majumbani au bila kuwepo ofisini na sera za ufanyaji kazi kutokea nyumbani na zana za kuwezesha kufanikisha hilo.

 

Vilevile, Kijitabu cha Mwongozo kwa Mwajiri kimegusia masuala ya mawasiliano yenye ufanisi na wafanyakazi, Usimamizi wa Utendaji wa Wafanyakazi na Ustawi pamoja na mkakati wa rasilimali watu baada ya janga la corona.

 

Kijitabu hiki kimeandaliwa kwa kutumia mjumuisho wa mbinu ikiwamo taarifa zilizokusanywa kutoka kwenye tafiti za nje, wataalamu wa Rasilimali watu wa Brighter Monday na wataalamu wa rasilimali watu kutoka kwenye makampuni mbalimbali nchini Tanzania.

 

Kitabu hiki kinakusudia kuwasaidia wale waliopo kwenye sekta ya usimamizi wa rasilimali watu wakati wa majanga na hata huko baadaye. Kinaweza kutumika kama mwongozo  wa kuweka dhana katika utendaji na kutengeneza mbinu zinazofaa zaidi katika eneo la kazi.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kijitabu hicho, Mkurugenzi wa BrighterMonday Tanzania Reshma Bharmal-Shariff amesema “Sote tunafahamu kuwa tulipita katika changamoto ambayo hatukuitarajia lakini pia haikuwahi kutoke kabla. Hii ilitufanya sisi kama wadau wa rasilimali watu kuona haja kubwa ya kutoa ushauri na maoni ya wataalamu mbalimbali katika sekta ya rasilimali watu.’’

 

Bi. Reshma ameongeza kuwa kitabu hiki kinalenga kusaidia watendaji na wadau wa rasilimali watu kufahamu mbinu na taratibu sahihi za kuongoza na kusimamia timu kwa ufasaha zaidi wakati wanapopata changamoto na hata baada. Vilevile, kitawawezesha Waaajiri na kuwasaidia waajiriwa kupata mwongozo wa kuboresha eneo la kazi. Vilevile, kitabu hiki kinawafaa hata wale wanaotafuta ajira kufahamu ni mchakato mzima wa uajiri.

 

Vilevile, Meneja Masoko wa BrighterMonday Tanzania, Erca Uisso alisema kuwa “kiijitabu hiki ni bure kwa kila mmoja na kinapatikana kwa mfumo wa nakala tepe inayopatikana kwenye tovuti ya Brighter Monday Tanzania kwa kutembelea kiungo hiki www.brightermonday.co.tz/research

 

Kuhusu Brighter Monday

BrighterMonday ilianzishwa mwaka 2012 kama jukwaa la kutafuta kazi na kusahili na hivi sasa imekuwa jukwaa lenye huduma zote za mchakato wa uajiri na usimamizi wa rasilimali watu ikiwamo kutoa ushauri wa ajira, huduma za kipekee za rasilimali watu kwa taasisi na watu binafsi na huduma ya mafunzo kwa waajiriwa na wanaotafuta ajira.

 

BrighterMonday inaaminika na kutoa huduma zake kwenye zaidi ya nchi 10 Afrika ikiwamo Tanzania, Kenya, Ethiopia, Uganda, Afrika Kusini, Nigeria, Senegal, Cameroon na Eritrea.