
Sanamu iliyokuwa
ikimuonesha Rais wa zamani wa Marekani, Abraham
Lincoln na mtumwa aliyeachiliwa huru akionekana kupiga magoti miguuni pake imeondolewa
katika kiunga chake jijini Boston.
Sanamu hiyo
ilizua mgogoro hivi karibuni kipindi ambacho Marekani ipo katika vuguvugu la
kupingana na ubaguzi wa rangi nchini humo. Sanamu hiyo imeondolewa mapema jumanne katika
viunga vya bustani ambapo ilikuwa imesimama tangu mwaka 1879.
Sanamu hiyo Iliundwa kusherehekea mwisho wa utumwa huko Marekani na ilimuhusisha Mtu mweusi, Archer Alexander mtumwa aliyetoroka utumwa alisaidia Jeshi la Muungano na alikuwa mtu wa mwisho kutumikishwa chini ya Sheria ya Mtumwa Mkimbizi.
Zaidi ya watu 12,000 walikuwa wamesaini ombi kutaka sanamu hiyo iondolewe, na tume ya sanaa ya umma jijini Boston ilipiga kura ya siri kuiondoa.
Sanamu hiyo ilitakiwa kuhifadhiwa hadi jiji litakapoamua ikiwa itaonyeshwa kwenye jumba la makumbusho.
Sherehe za kumbukumbu za sherehe hizo zilikuwa zikifanyika hadi ilipotimu mnamo 2008 ambapo ilizindua tathmini kamili kuhakikisha sanamu za umma, makaburi na kazi zingine za sanaa hazichochei ubaguzi wa rangi.
Tume ya sanaa jijini humo ilisema ilikuwa ikizingatia kazi za sanaa ambazo historia yake inaonekana kuwa na matatizo.
Lakini wakati wengine walimwona yule mtu asiye na shati akiinuka kwa miguu yake huku akitikisa pingu zilizovunjika kwenye mikono yake ni mtumwa mbele ya Lincoln, Baadhi ya watu wamesema hakukua na shida kwenye sanamu hiyo kwani Rais Lincoln ndiye aliyekomesha Utumwa nchini Marekani na Sanamu hiyo ni kumbukumbu ya tukio hilo.
Leave a comment