Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kituo cha utangazaji cha 255 Global Radio, Twenzao App, Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi, Mtangazaji wa Global TV, Anna Mbawala kwa pamoja wamepokea tuzo zao za Tanzania Digital Awards (TDA) ambazo zilianzishwa mwaka 2020 nchini Tanzania na kampuni ya Serengeti Bytes kwa lengo la kutambua juhudi za watu binafsi, mashirika, kampuni pamoja na Serikali katika kutumia teknolojia ya kidigitali kuleta mabadiliko chanya katika jamii.Tuzo hizo zimetolewa leo Mei 24, 2022 jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Bytes, Kennedy Mmari pamoja na Afisa uendeshaji wa Serengeti Bytes, Michael Mallya.Mkurugenzi wa LHRC, Wakili Anna Henga pamoja na baadhi ya watumishi wa kituo hicho wamepokea tuzo hiyo baada ya LHRC kushinda katika kipengele cha uvumbuzi bora wa namna ya kufikisha Haki kwa kutumia teknolojia ya kidigitali (2021) kwa kutumia Aplikesheni yake ya Haki kiganjani.Pia, LHRC imepokea tuzo yake ya Mwaka 2020 ambayo ilishinda katika kipengele cha Azaki bora kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii.Katua hatua nyingine, Aplikesheni ya usafiri ya Twenzao APP imepokea tuzo yake ya mwaka 2021 baada ya kushinda katika kipengele cha uvumbuzi bora wa kidigitali katika kurahisisha huduma za usafirishaji. Tuzo hiyo imepokelewa na mwanzilishi wa Twenzao App, Bw. Amo Mushumbusi pamoja na Afisa Mkuu uendeshaji wa Twenzao App, Bw. Amos Richard.Kituo cha Redio ya mtandaoni cha 255 Global Radio kilicho chini ya Global Group kimepokea tuzo yake ya mwaka 2021 iliyoshinda katika kipengele cha redio bora ya mtandaoni.Pia, mtangazaji wa Global TV, Anna Mbawala amepokea tuzo yake ya mwaka 2021 aliyoshinda katika kipengele cha mwanahabari bora wa kidigitali (Manamke).Pia, Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ya Msichana Initiative, Rebeca Gyumi amepokea tuzo yake ya mwaka 2021 ya Kiongozi bora (mwanamke) kutoka Asasi za Kiraia kwenye matumizi bora ya mitandao ya kijamii hususani katika kutetea haki za wasichana nchini Tanzania. Aidha, Mkurugenzi wa LHRC, Wakili Anna Henga amepokea tuzo yake ya mwaka 2020 aliyoshinda katika kipengele cha Kiongozi bora (mwanamke) kutoka Asasi za Kiraia kwenye matumizi bora ya mitandao ya kijamii.
Serikali ya nchi ya Gambia imetangaza kumfungulia mashtaka ya mauaji, ubakaji,utekaji na utesaji wa raia, ufisadi, rushwa na makosa mengine aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Bw. Yahya Jammeh. Makosa hayo aliyatenda akiwa madarakani kati ya mwaka 1994 hadi 2017.Akitoa taarifa hiyo jana Mei 25, 2022, Waziri wa Sheria wa nchi hiyo amesema kuwa serikali imepokea mapendekezo ya ripoti ya Kamati ya ukweli, maridhiano na uponyaji na kukubali kuyatekeleza mambo 263 kati ya 265 yaliyopendekezwa ikiwa ni pamoja na kumshtaki kiongozi huyo aliyepo uhamishoni nchini ‘Equatorial Guinea.’Waziri huyo wa sheria amesema kuwa wengine watakaoshtakiwa sambamba na Jammeh ni aliyekuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Isatou Njie-Saidy na pamoja na washirika wake wengine wa karibu wakiwepo wanausalama waliokuwa kwenye kikosi cha Jammeh kilichohusika na utekaji na utesaji na mauaji huku kikijulikana kama “Junglers hit squad.”Katika ripoti hiyo iliyokabidhiwa kwa Rais Adam Barrow na kuwekwa hadharani mnamo mwezi Disemba 2021 ilitumia muda wa miaka 2 kukamilisha kukusanya uchunguzi na ushahidi wa wahanga wa Utawala wa Rais Jammeh akiwa madarakani. Aidha, ikumbukwe kuwa Rais Jammeh yupo uhamishoni katika nchi ambayo haina mkataba wa kubadilishana wahalifu na nchi yake ya Gambia, hivyo wananchi wanahoji Je, itakuwaje kumpata ili aje kuwajibishwa?